Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Dkt. Akjeman Magtgmova, Mwakilishi wa WHO nchini Syria akiwa amembeba mtoto kwenye moja ya kituo cha afya nchini humo.

UN imelaani vikali shambulio la kutisha hospitali nchini Syria

WHO Syria
Dkt. Akjeman Magtgmova, Mwakilishi wa WHO nchini Syria akiwa amembeba mtoto kwenye moja ya kituo cha afya nchini humo.

UN imelaani vikali shambulio la kutisha hospitali nchini Syria

Amani na Usalama

 Maafisa wakuu wa Umoja wa Mataifa leo wamelaani vikali shambulio baya lililofanyika katika hospitali nchini Syria mwishoni mwa wiki na kusisitiza haja ya uwajibikaji kwa uhalifu uliofanywa katika vita vya miaka kumi vya nchi hiyo. 
 

Hospitali ya Al-Shifaa imeshambyuliwa wakati wa uvurumishaji wa makombora katika mji ulioshikiliwa na waasi kaskazini mwa Afrin siku ya Jumamosi. 
Takriban raia 18 waliuawa, kulingana na ripoti za vyombo vya habari, pamoja na wafanyikazi na wagonjwa hospitalini, pia sehemu ya kituo hicho cha afya iliharibiwa. 
Kusitisha uhasama kunahitajika sasa 
"Mashambulio hayo ya kutisha kwa raia na miundombinu ya raia, pamoja na vituo vya huduma za afya na wafanyikazi, hayakubaliki na lazima yakomeshwe", amesema mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwa aji9li ya Syria, Geir Pedersen, katika taarifa  yake iliyotolewa leo Jumatatu. 
 
 Ameongeza kuwa “Pande zote kinzani katika mzozo wa Syria lazima zitii kikamilifu majukumu yao chini ya sheria za kimataifa za kibinadamu, pamoja na ulinzi wa raia na vitu vya raia. Ninasisitiza tena wito wa Katibu Mkuu wa uwajibikaji kwa uhalifu uliofanywa nchini Syria. " 
Mjumbe huyo amesema kuwa shambulio hilo, na kuendelea na ghasia huko Syria, kunasisitiza tena umuhimu wa kutekeleza usitishaji mapigano kitaifa, na pia juhudi mpya kuelekea suluhu ya kisiasa katika taifa hilo la Mashariki ya Kati. 
 
Shambulio la tatu katika miaka miwili 

Hospitali ya Al-Shifaa, moja ya vituo vikubwa vya afya kaskazini mwa Syria, imekumbwa na mashambulizi mara tatu tangu 2019, kulingana na maafisa wakuu wawili wa Umoja wa Mataifa. 
 
Imran Riza, mratibu mkazi na mratibu wa masuala ya kibinadamu wa nchi hiyo, na Muhammad Hadi, mratibu wa masuala ya kibinadamu wa kikanda wa kwenye mgogoro wa Syria, wamelaani vikali shambulio hilo katika taarifa ya pamoja iliyotolewa Jumapili. 
 
Wamesema hospitali hiyo hutoa wastani wa huduma za matibabu kwa wagonjwa 15,000 kila mwezi, pamoja na kujifungua watoto wachanga 350 na huduma ya upasuaji maalum 250.  
 
Imekuwa ikipokea msaada wa kifedha kutoka kwa Umoja wa Mataifa kwa miaka miwili iliyopita. 
"Kwa watu wa Syria, ambao tayari wameathirika vibaya na miaka kumi ya shida kutokana na vita, vituo vya afya vinapaswa kuwa mahali salama", taarifa yao ilisema. 
 
Wamesisitiza kuwa kuelekeza mashambulizi dhidi ya raia na miundombinu ya raia, ikiwemo hospitali, ni marufuku kabisa chini ya sheria za kimataifa ya kibinadamu.