Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mabadiliko ya tabianchi ni janga kwa wafugaji Uganda

Mabadiliko ya tabianchi ni janga kwa wafugaji Uganda

Pakua

Mabadiliko ya tabianchi ni janga ambalo linaikabili dunia hii leo ambapo Umoja wa Mataifa na washirika wake kupitia lengo nambari 13 la ajenda ya mwaka 2030 ya maendeleo endeleve au SDGs, wamekuwa msatari wa mbele kubonga bongo ili  kutafuta suluhisho ikiwa ni pamoja na  kuhamisha serikali na asasi mbalimbali kuweza kutafuta njia mbadala ya kupambana na janga hili.

Katika miaka ya hivi karibuni Mashariki mwa bara la Afrika kumekuwa kukikumbwa na tatizo la mabadiliko ya tabianchi ambayo yamesababisha ukame, maporomoko ya ardhi na mafuriko. Katika makala hii mwandishi wetu John Kibego, kutoka Uganda amefuatilia hali ya ukame katika wilaya ya Bulisa nchini humo ambayo imesababisha ukosefu wa malisho  kwa wafugaji hivyo kufanya mifugo mingi kufa  nakusababisha umasikini kwa jamii hii ya mashinani.

Kwa undani zaidi kuhusu nini kilichojiri ungana naye katika makala hiii.

Audio Duration
3'48"
Photo Credit
FAO