Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

 IFAD yawajenga mnepo wakulima nchini Ethiopia.

 IFAD yawajenga mnepo wakulima nchini Ethiopia.

Pakua

Zaidi ya watu bilioni moja kote duniani wanaishi katika maeneo ambayo yana uhaba mkubwa wa maji, na watu wengine wapatao bilioni 3.5 watakabiliwa na changamoto kubwa ya uhaba wa maji ifikapo mwaka 2025 kwa mujibu wa takwimu za shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO na shirika la maendeleo ya kilimo IFAD.

Miongoni mwa nchi zilizo na shida ya maji hususani wakati wa kiangazi kwa wakulima vijijini kutokana na mabadiliko ya tabianchi ni Ethiopia, lakini sasa mradi wa umwagiliaji wa IFAD umeleta nuru kwa wakulima wengi wa taifa hilo la Pembe ya Afrika akiwemo Boru Gudo ambaye anazungumzia jinsi gani mradi huo umemfanya yeye na familia yake waweze kuishi na kupata kipato wakati wa kipindi cha ukame mkali. Kwa undani zaidi ungana na Flora Nducha kwa Makala hii.

Audio Duration
3'6"
Photo Credit
UNICEF/Mulugeta Ayene