Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

UN News/George Musubao

Ingawa kuna changamoto najitahidi kutunza familia yangu- Tsinduka

Hii leo ni siku ya kimataifa ya familia duniani ambapo maudhui ya mwaka huu ni mienendo ya makundi ya watu na familia wakati huu ambapo idadi ya watu inaongezeka ingawa kwa kiwango cha chini. Umoja wa  Mataifa unasema kupungua kwa idadi ya wanafamilia hutoa fursa ya familia kupatia huduma bora zaidi watoto, mathalani elimu na afya.

Audio Duration
4'26"
Stella Vuzo/UNIC Dar es Salaam

Khadija Khalid Ismail na Ebenezer Suleiman Mathew kuwawakilisha vijana wa Tanzania katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa

Mwezi Septemba mwaka huu wakuu wa serikali na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kama ilivyo ada ya kila mwaka watakutana katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani kujadili masuala mbalimbali ya Ulimwengu.  

Wakati wa mkutano huu wa juu kabisa katika Diplomasia ya Umoja wa Mataifa, vijana pia hushiriki katika mikutano ya kando ili kuchangia mawazo yao katika mstakabali wa ulimwengu.  

Vijana wawili kutoka Tanzania Khadija Khalid Ismail na Ebenezer Suleiman Mathew watawakilisha vijana wenzao wakati wa Baraza hili.  

Sauti
2'37"
© UNICEF/Veronica Houser

Jamii msimkatae msichana akipata ujauzito bila kutarajia. Si mwisho wa maisha - Ashley Toto

Ripoti iliyopewa jina Kuzaliwa kabla ya wakati: muongo wa hatua dhidi ya kuzaliwa kabla ya wakati, iliyotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) pamoja na PMNCH ambao ni Ushirikiano wa mkubwa zaidi unaoangazia Afya ya Mama, watoto na vijana inaeleza kwamba mwaka 2020 takriban watoto milioni 13.4 duniani walizaliwa kabla ya wakati yaani njiti, huku karibu milioni 1 kati yao wakifariki kutokana na matatizo yanayotokana na hali hiyo ya kuzaliwa kabla ya wakati. 

Sauti
4'44"
UN News/George Musubao

Uhuru wa kujieleza kama kichocheo cha haki zote za binadamu

Hii leo ikiwa ni siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani maudhui yakiwa Kuumba mustakabali wa Haki: Uhuru wa kujieleza kama kichocheo cha haki zote za binadamu tunakwenda Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako huko mwandishi wetu George Musubao amezungumza na waandishi wa habari kufahamu uzingatiaji wa maudhui ya siku hii halikadhalika kile ambacho wangependa kuona kinafanyika ili haki hiyo ya kupata habari iweze kuzingatiwa na hatimaye iwe kichocheo cha wananchi kupata haki zote.

Sauti
6'28"
TANBAT 6

Mwambata wa jeshi wa Tanzania nchini atembelea Kikosi cha Tanzania TANBAT 6 wanaohudumu chini ya MINUSCA nchini CAR.

Mwambata jeshi wa Tanzania anayehudumu kazi yake Jamhuri ya Afrika ya kati Brigedia Jenerali Absolomon Lyanga Shausi amefanya ziara ya kutembelea kikosi cha walinda amani wa Tanzania TANBAT6 wanaohudumu chini ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati MINUSCA ili kujitambilisha tangu kikosi hicho kianze shughuli ya ulinzi wa amani kikipokea majukumu kutoka kwa kikosi cha TANBAT5 mwishoni mwa mwaka.

Kapteni Mwijage Inyoma aliyeko nchini Afrika ya Kati anaeleza zaidi..

Sauti
2'31"
UN News

Jukwaa la vijana limetukutanisha na watunga sera za mataifa mbalimbali

Tayari tangu jana Aprili 25, Jukwaa la Vijana la Baraza la Umoja wa Mataifa la Kiuchumi na Kijamii (ECOSOC) la mwaka 2023 limeng’oa nanga ambapo maelfu ya viongozi vijana kutoka duniani kote wanakusanyika katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York kujadili pamoja na mambo mengine, masuala yanayolenga kuharakisha kujikwamua kutoka janga la COVID-19 na utekelezaji kamili wa Ajenda ya 2030 ya Malengo ya Maendeleo Endelevu. 

Sauti
3'39"