Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jamii msimkatae msichana akipata ujauzito bila kutarajia. Si mwisho wa maisha - Ashley Toto

Jamii msimkatae msichana akipata ujauzito bila kutarajia. Si mwisho wa maisha - Ashley Toto

Pakua

Ripoti iliyopewa jina Kuzaliwa kabla ya wakati: muongo wa hatua dhidi ya kuzaliwa kabla ya wakati, iliyotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) pamoja na PMNCH ambao ni Ushirikiano wa mkubwa zaidi unaoangazia Afya ya Mama, watoto na vijana inaeleza kwamba mwaka 2020 takriban watoto milioni 13.4 duniani walizaliwa kabla ya wakati yaani njiti, huku karibu milioni 1 kati yao wakifariki kutokana na matatizo yanayotokana na hali hiyo ya kuzaliwa kabla ya wakati. 

Aidha miongoni mwa sababu zinazotajwa na ripoti hiyo kuwa zinachangia kwa kiasi kikubwa watoto kuzaliwa njiti ni pamoja na mimba za utotoni na shinikizo kubwa la damu wakati wa ujauzito (pre-eclampsia). Katika muktadha huo Anold Kayanda anatupeleka nchini Kenya kumwangazia mama mwenye umri mdogo Ashley Toto akieleza changamoto alizozipitia kutokana na kujifungua mtoto njiti. 

Audio Credit
Selina Jerobon/Anold Kayanda
Audio Duration
4'44"
Photo Credit
© UNICEF/Veronica Houser