Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

Picha: Video screenshot

Mradi wa Sports for Protection unanisaidia kuondoa msongo wa mawazo na kuniepusha na wadanganyifu – Yomjima Konyi Kurok

Sports for Protection ni mbinu ya kutumia michezo kwa ajili ya kusaidia maendeleo na ulinzi wa vijana waliofurushwa au walioko ukimbizini ni mkakati ulioanzishwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR kwa kushirikiana na Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki na sasa unatekelezwa na mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa kama la idadi ya watu duniani na masuala ya afya ya uzazi UNFPA Kenya kwa kushirikiana na tasisi nyingine za kitaifa na kimataifa. Selina Jerobon wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa anasimulia zaidi kupitia makala hii.

Sauti
3'5"
Picha: WHO Video screenshot

WHO na wadau waingilia kati kupambana na utapiamlo mkali unaosababishwa na athari za ukame Pembe ya Afrika

Ukame katika ukanda wa Pembe ya Afrika umeleta madhara makubwa kwa ustawi wanadamu na ikolojia nzima katika eneo hilo. Madhara ya moja kwa moja yaliyoshuhudiwa na watu wa ukanda huo zikiwemo nchi za Somalia, Kenya, Ethiopia na maeneo ya kaskazini mwa Uganda ni ukosefu wa chakula na hivyo kusababisha utapiamlo hasa utapiamlo mkali kwa watoto.

Mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwemo la Afya Ulimwenguni, WHO na wadau wake, wameingilia kati ili kupunguza makali ya tatizo hilo kama si kulimaliza kabisa. Anold Kayanda ameangazia hatua hizo na kutuandalia makala ifuatayo.

Sauti
3'3"
©Education Cannot Wait

Vijana wa Berberat nchini CAR wakabidhiwa mradi wa madarasa yatakayotumika kutoa elimu ya kompyuta na TEHAMA: TANZBATT 6

Mkuu wa kikosi cha 6 cha Walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania wanaohudumu chini ya MINUSCA, Luteni Kanali Amini Steven Mshana amefungua na kukabidhi madarasa yatakayotumika kutoa elimu ya kompyuta na TEHAMA kwa ujumla kwa vijana wa eneo la mji wa Berberat na viunga vyake ili kuwapa ujuzi wawe na mchango chanya kwa jamii yao badala ya kujiunga na makundi ya waasi.Kapteni Mwijage Francis Inyoma ni Afisa Habari wa TANZBATT 6 anaripoti.

Sauti
2'44"
Picha: UN News

Lengo la ujumuishi kwenye elimu na kutomwacha mtu yeyote nyuma ladhihirika Tanzania

Umoja wa Mataifa unatambua kuwa elimu ina uwezo mkubwa wa kumuinua mtu kiuchumi na kijamii, kwa maana ya kwamba ni silaha mujarabu ya kuondokana na umaskini. Kupitai malengo ya maendeleo endelevu, SDGs, hususan lengo namba 4, Umoja wa Mataifa unataka elimu bora tena isiyomwacha mtu yeyote nyuma, kwa misingi ya rangi, eneo aliko au hali ya mwili wake. Tayari nchi na mashirika ya kimataifa na yasiyo ya kiserikali yanafanikisha lengo hilo, mfano humo nchini Tanzania katika mkoa wa Morogoro ulioko mashariki mwa taifa hilo la Afrika. 

Sauti
5'3"
UN News

Mradi wa PLEAD wawezesha huduma za mahamaka kupatikana muda wote nchini Kenya

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya madawa na uhalifu UNDOC kanda ya Afrika Mashariki kwa kushirikiana na sekta ya mahakama nchini kenya wamepanga kuanza kutekeleza awamu ya pili ya mradi wa uwekaji umeme wa sola katika mahakama na magereza nchini humo baada ya awamu ya kwanza kuonesha mafanikio.

Kupitia mradi ujulikanao kama PLEAD unaofadhiliwa na Muungano wa Ulaya UNODC na sekta ya mahakama nchini Kenya wamefanikiwa kutekeleza mradi wa awamu ya kwanza katika mahakama mbili zilizoko Mombasa ambazo zilikuwa zikishindwa kuendesha shughuli zake pindi umeme unapokatika.

Sauti
3'23"
IAEA Video

Teknolojia ya nyuklia yaleta matumaini kwa wakulima nchini Kenya

Je ni kwa vipi teknolojia ya nyuklia inaweza kuleta tofauti katika uzalishaji wa chakula wakati huu ambapo janga la tabianchi linazidi kugonga vichwa vya watu na kubisha hodi kila uchao? Baadhi ya watu wakisikia nyuklia kinachowajia kichwani ni mabomu ya nyuklia, lakini nchini Kenya, wanasayansi na wakulima wanaelezea kwa maneno yao wenyewe vile ambavyo sayansi ya nyuklia inasaidia kupambana na uhaba wa chakula na maji. Kuanzia uzalishaji wa mbegu mpya zinazohimili ukame hadi teknolojia za kutambua ni muda gani muafaka kumwagilia mazao.

Sauti
4'43"