Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

UNMISS

Wananchi wa Sudan Kusini washerehekea tamasha la utamaduni la amani

Mwanzoni mwa mwezi huu wa April dunia iliadhimisha Siku ya Kimataifa ya michezo kwa maendeo na amani, nchini Sudan Kusini kwa siku mbili mfululizo maelfu ya wananchi walikusanyika kusherehekea tamasha la utamaduni la amani lililoandaliwa na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS kwa kushirikiana na Wizara ya Utamaduni ya jimbo la Kaskazini la Bahr El Ghazal.

Maelfu ya wananchi walikusanyika kwa ajili ya sherehe hizo katika mji wa Aweil, wakitazama na kushiriki kuimba na kucheza nyimbo na ngoma za kitamaduni. Leah Mushi anasimulia hali ilivyokuwa

Sauti
4'27"
UN News/Florence Westergard

Nguo hizi za binti yangu ni ushahidi tosha kuwa mauaji ya kimbari yapo: Manusura mauaji ya Rwanda

Katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa kunafanyika maonesho yaliyopatiwa jina Simulizi za Manusura na Kumbukizi: Wito wa kuchukua hatua kuzuia mauaji ya kimbari. Katika maonesho haya vifaa mbali mbali vinavyohusiana na mauaji ya kimbari, mathalani ya Rwanda au kule Bosnia Hezergovina na Srebenica vinaoneshwa, yakiwemo mavazi ya wale waliokumbwa na mauaji hayo. Mauaji ya kimbari nchini Rwanda yalifanyika kwa siku 100 kuanzia Aprili 7 hadi Julai 15 mwaka 1994. Hadi leo hii manusura na wale waliopoteza ndugu na jamaa zao bado machungu yako moyoni mwao na wanatumia maonesho haya kupata sauti.

Sauti
4'39"
UN News

Athari za utupaji wa taka za plastiki kwenye maziwa na baharí

Uchafuzi wa mazingira katika maeneo ya bahari unatajwa kuwa na athari kwa viumbe hai waishio chini ya maji kutokana na baadhi ya taka ikiwemo plastiki kuwa na madhara ya moja kwa moja kwa viumbe hao.

Umoja wa Mataifa umekuwa ukizitaka nchi wanachama kuhakikisha wanadhibiti taka hizo katika mataifa yao ili kuokoa Maisha ya viumbe hai waishio chini ya maji pamoja na mfumo wa Ikolojia.

Sauti
3'5"
Chadron's Hope Foundation/Elly Kitally

Nimejifunza watu wenye Down Syndrome wanaweza kuishi maisha ya kawaida wakijumuishwa – Elly Kitaly

Hivi karibuni katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa umefanyika mkutano wa Siku ya Kimataifa ya Down Syndrome. Mkutano huo uliokuwa na kauli mbiu “Pamoja nasi, kwa ajili yetu” uliandaliwa na taasisi ya Down Syndrome International (DSI) kwa kushirikiana na taasisi ya The International Disability Alliance (IDA), Uwakilishi wa kudumu katika Umoja wa Mataifa wa Brazil, Japan na Poland.  

Sauti
3'14"
UN News/Anold Kayanda

MuDa Africa washindi wa ufadhili wa UNESCO wahamasisha wasichana kutoficha vipaji vyao

Wasanii kutoka Taasisi ya Muda Africa ya nchini Tanzania, kundi ambalo ni washindi wa ufadhili wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) wanatoa wito kwa wasichana na wanawake kutoficha vipaji vyao ili waweze kutimiza ndoto zao na jamii iwasaidie kuyatimiza malengo hayo kwani hiyo itasaidia kuondoa pengo la usawa wa kijinsia katika tasnia mbalimbali ambazo kwa muda mrefu zinahodhiwa na wanaume.

Sauti
4'4"
UNICEF

Hakikisho la maji safi na salama lachochea jamii kuishi na utangamano Mkoani Kigoma nchini Tanzania

Ufumbuzi wa ubunifu wa maji unaotumia teknolojia ya nishati ya jua ambao unafanikishwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kwa kushirikiana na wadau wake ukiwemo ule wa utekelezaji, Water Mission, na ule wa kutoa msaada wa fedha Grundfos Foundation kutoka nchini Denmark umesaidia serikali ya Tanzania kubuni suluhisho la msingi na la kudumu la maji katika jamii 15 za mkoa wa Kigoma ulioko magharibi mwa taifa hilo la Afrika Mashariki. Lengo lao kubwa ni kuhakikisha upatikanaji wa maji safi na salama kwa watu 99,107 mkoani humo ifikapo Machi 2024. 

Sauti
5'48"
UN News/Assumpta Massoi

Vijana ni wakati wetu sasa kufanikisha upatikanaji wa maji- Laurel

Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu maji ulifanyika kwa siku tatu kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani kuanzia tarehe 22 mwezi huu wa Machi. Mkutano huu ulichukuliwa kama fursa ya kipekee ya kizazi hiki ya kuharakisha maendeleo kuelekea upatikanaji wa maji salama na usafi wa mazingira ifikapo mwaka 2030 kwa kuzingatia kuwa mara ya mwisho ya mkutano kama huu kufanyika ilikuwa mwaka 1977.

Sauti
4'48"