Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

UN/ Jason Nyakundi

Mtaani hakuna kazi lakini kuna fursa tutumie tujikwamue – Dorcas 

Kijana Dorcas Mwachia anakaribia kuhitimu shahada ya uzamili huko nchini Kenya. Ingawa hivyo katika kuelekea kutamatisha safari yake amegundua kuwa hana uwezo kifedha wa kumalizia karo na njia pekee ni kubonga bongo ajikwamue yeye na nduguye. Pitapita ya mitaa ya Nairobi nchini Kenya ikamkutanisha na chupa zilizotumika ambazo kwake yeye akaona ni fursa, huku akisafisha mazingira na wakati huo huo anazitumia kutengeneza mapambo anayouza. Kipato mfukoni na mazingira yanakuwa safi na sasa ameweza kukamilisha karo ya Chuo Kikuu na mengine mengi.

Sauti
3'8"
Warren Bright/UNFPA Tanzania

Kijana wa kiume apazia hatua dhidi ya ukeketaji nchini Kenya

Mila potofu ya ukeketaji watoto wa kike na wanawake bado imeendelea kujikita katika jamii mbalimbali duniani licha ya nuru kuonekana katika baadhi ya maeneo kuwa ukeketaji unaanza kufifia. Umoja wa Mataifa unasema kuwa mwaka 2019 wasichana milioni 4.1 walikuwa hatarini kukeketwa na kutokana na makadirio ya ongezeko la idadi ya watu, idadi hiyo inaweza kufikia milioni 4.6 mwaka 2030.

Sauti
3'40"
UN News

Wanajamii tulindane wakati wa sikukuu na hasa ulinzi kwa watoto - Mwanaharakati wa haki za wanawake Uganda

Katika shamrashamra za siku kuu watoto huwa hatarini kwa namna mbalimbali. Bi. Monica Kabakwonga, mwanaharakati wa haki za wanawake na pia mwenyekiti wa kikundi cha Tukorre Hamo Women’s Group cha nchini Uganda anawachagiza wazazi kuimarisha ulinzi wa watoto dhidi ya mabaya yote ukiwemo ugonjwa wa Covid-19.  Pata maelezo zaidi kwa kusikiliza makala ifuatayo ambapo mwandishi wetu John Kibego anazungumza na mwanaharakati huyo.

Sauti
3'9"
© FAO-Magnum Photos/Alex Webb

Tunataka kubadilisha mtazamo wa watu warejee katika vyakula vya kienyeji - Miriam Nabakwe

Umoja wa Mataifa uliutangaza mwaka huu wa 2021 unaoelekea ukingoni kuwa mwaka wa mbogamboga na matunda lengo likiwa ni kuelimisha watu kuhusu umuhimu na faida za mbogambona na matunda mwilini. Miriam Nabakwe wa nchini Kenya anasema tatizo hilo la watu kutokula mbogamboga lipo na mbaya zaidi ni kuwa hata vyakula ambavyo watu sasa wanavithamini si vile vya asili na hivyo kuongeza tatizo juu ya tatizo kwani anaamini vyakula vya asili vilivyosalia katika maeneo mbalimbali duniani ndivyo vyenye virutubisho asilia.

Sauti
3'34"
UNICEF TANZANIA

Najivunia kuwa mfanyakazi wa UNICEF Tanzania kwa karibu miaka 20:Said Mumba

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF mwezi huu limetimiza miaka 75 tangu kuanzishwa kwake rasmi tarehe 11 Desemba 1946 jijini New York Marekani kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa. 

Na kwa miaka 75 limekuwa likitoa huduma mbalimbali za kibinadamu na misaada ya maendeleo kwa watoto katika maeneo na nchi 192 na ni moja ya mashirika yanayotambulika na kuthaminiwa kote duniani. 

Sauti
2'5"
UNEP

Mshindi wa tuzo ya mazingira wa UNEP 2021 kutoka Uganda azungumzia kazi anazofanya

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa mazingira duniani, UNEP wiki hii Jumanne ya tarehe 07 limewatangaza washindi wanne wa tuzo yake ya juu kabisa ya mazingira ijulikanayo kama “champions of the Earth Award” kwa mwaka 2021. Mabingwa hao walichaguliwa kutokana na mchango katika mazingira na uongozi wao katika kuendeleza hatua za ujasiri na madhubuti kwa niaba ya watu wengine wa sayari dunia. Dk Gladys Kalema-Zikusoka wa Uganda ni mmoja wa tuzo hiyo ya UNEP katika kipengele cha Sayansi na Ubunifu.

Sauti
3'39"
© UNICEF/Jimmy Adriko

Uganda nayo yachukua hatua kuimarisha matumizi ya lugha ya Kiswahili

Tarehe 23 mwezi uliopita wa Novemba mwaka huu wa 2021, Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO liliridhia tarehe 7 mwezi Julai kila mwaka kuwa siku ya kimataifa ya Kiswahili. 
 
Hatua hii imezingatia misingi mbalimbali ikiwemo nafasi ya lugha hiyo katika kuleta utangamano katika jamii, kuwa chanzo cha kipato na hata kusongesha amani na usalama. 
 

Sauti
4'6"
World Bank/Flore de Preneuf

Kijana mwanamazingira Rebecca Laibich ajitolea kufundisha wengine

Katika makala hii leo tunajiunga na mwandishi wetu wa Kenya Jason Nyakundi akizungumza na Rebecca Laibich, kijana mwenye umri wa miaka 25 mwanaharakati wa kuhifadhi mazingira nchini Kenya na mfanyakazi wa kujitolea wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO, ambaye amejitwika jukumu la kuwafunza vijana wenzie kuhusu umuhimu na njia za kutunza mazingira.

Sauti
3'20"