Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

Picha: Kwa hisani ya James Waikibia

Maji safi na maji taka vyote ni changamoto Nairobi Kenya

Uondoaji  wa maji taka na upatikanaji wa maji safi ya kunywa vyote ni changamoto kubwa ambayo inakumba sehemu  nyinyi na hasa miji ya nchi za Afrika. Kila mara mabomba ya maji taka hupasuka na kuvuja ambapo na ukarabati wa miundo mbinu muhimu kama hiyo  huchukua muda mrefu na wakati mwingine kutelekezwa kabisa.

Sauti
4'32"
UN News/Elizabeth Scaffidi

Kufanya kazi kwa vitendo ni moja ya vitu vilivyonisaidi kufikia nilipofika maishani-Kijana Katuma

Kijana Richard Katuma ni mmoja wa vijana ambao kwa wakati mmoja alikuwa ni mchanigaji wa vipindi vyetu kwenye Idhaa ya Kiswahili ya UN News alipokuwa akifanya kazi na moja ya radio washirika, lakini kama anavyosimulia katika mahojiano na Assumpta Massoi wa Idhaa hii mabadiliko katika maisha yalimlazimu yeye kubadili mtindo wa maisha. Hatahivyo kuna baadhi ya mambo ikiwemo kufanya kazi kwa vitendo ambayo anasema yalimsaidia yeye katika kufanikisha masomo yake lakini pia kupata ajira. Kulikoni? Basi ungana naye katika makala hii.

Sauti
3'47"
UN Environment/Jack Kavanagh

NEMA Kenya kwa kutambua athari za uchafuzi wa hali ya hewa imechukua hatua

Uchafuzi wa hewa unasababishwa na chemichemi haribifu ambazo zinasambaa hewani na athari zake ni mbaya kwani husababisha vifo vya mapema kutokana na magonjwa kama ya moyo, saratani pamoja na magonjwa ya matatizo ya kupumua.

Kwa mujibu wa shirika la afya ulimwenguni uchafuzi wa hewa ulisababisha vifo milioni 7 kimataifa mwaka 2016. Huku vifo vingi vikitokea katika nchi zinazoendelea ambako sheria ni dhaifu au hazitekelezwi, uchafuzi wa hewa na magari yanayochagua mazingira havifuatiliwi.

Sauti
4'10"
UN News

Ingawa tumevunjwa moyo hatujakata tamaa na mabadiliko ya tabianchi:Fazal

Kutoafikiana kwa mataifa yanayochangia kiasi kikubwa cha hewa ukaa kwenye mkutano wa mabadiliko ya tabianchi au COP25 uliohitimishwa mwishoni mwa wiki, kumezifadhaisha nchi zinazoendelea ikiwemo bara la Afrika ambalo si mchangiaji mkubwa wa hewa ukaa lakini ni muathirika mkubwa wa athari zake. Changamoto ilikuwa ni ibara ya 6 inayojikita na biashara ya hewa ukaa. Katika makala hii Flora Nducha anazungumza na Fazal Issa mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya kumbukumbu ya Sokoine nchini Tanzania na pia mratibu wa makundi tisa yaliyo chini ya shirika la Umoja wa Matifa la mazingira UNEP.

Sauti
4'10"
Picha ya UN /Martine Perret

Ukikusanya chupa kulinda mazingira utazawadiwa:Inuka Foundation

Chupa na hasa la plastiki imekuwa moja ya tatizo kubwa la uchafuzi wa mazingira duniani na juhudi zinafanyika katika ngazi mbalimbali kuhakikisha taka hizo haziendeleo kuzagaa au kuishia baharini. Umoja wa Mataifa na wadau wako msitari wa mbele kuzichagiza jamii kuja na mbinu ya kupunguza taka hizo ikiwa ni pamoja na zile za kuzirejea na kutengeneza vitu vingine. Shirika la Inuka Foundation lililo na ofisi zake mjini Nairobi ni miongoni mwa wanaharakati hao wa mazingira  waliojitwika jukumu la kuhakikisha utunzi wa mazingira na hasa ukusanyaji wa taka za plastiki.

Sauti
4'
UNICEF/UNI212587/Tremeau

Usawa wa kijinsia si mwanamke kumkalia mwanaume bali kuweka uwiano wa maelewano kwa maslahi ya familia na jamii

Siku 16 za kupinga ukatili dhidi ya wanawake zikiwa zimefikia ukingoni wiki hii, tumekwenda mkoani Geita nchini Tanzania ambako asasi ya kiraia ya Women's Promotion Centre inaendesha harakati za kupigania utu na haki za msingi za wanawake katika maeneo ya kanda ya ziwa nchini humo. Asasi hiyo inalenga kufanikisha uelewa na heshima kwa haki na utu wa wanawake ili waweze kuwa na jamii inayosimamia usawa wa jinsia.

Sauti
6'2"
UNDP/Sawiche Wamunza

Mradi wa matumizi bora ya ardhi Tanga na Pwani Tanzania ni wa mfano- Jerome Nchimbi

Miongoni mwa hatua zinazochukuliwa hivi sasa na Umoja wa Mataifa ni kushirikiana na nchi wanachama katika kulinda, kutunza na kuendeleza ipasavyo vyanzo vya maji wakati huu ambapo matumizi holela ya vyanzo hivyo ni sababu kuu ya madhara ya mabadiliko ya tabianchi. Mathalani kilimo kisichozingatia mipango katika vyanzo husababisha maji kukauka na wakazi kusalia bila maji.

Sauti
4'15"
UN Women

Pombe zilizoongezwa nguvu Bukavu zachochea ukatili wa kingono jimboni Kivu Kusini

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC,  vitendo vya ukatili wa kingono hususan ukatili majumbani huko DRC ukitambulika kama ujeuri wa kijinsia vimekuwa mwiba kwa maendeleo ya jamii,hususan wanawake, wasichana na watoto. Watoto wanakimbia nyumbani, wanawake wanatoa mimba na moja ya sababu ni wanaume kunywa pombe zilizoongezwa nguvu zaidi na hatimaye kupiga familia zao.

Sauti
3'40"