Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala: Mchoro wa Ashraf Kuku waibuka kidedea kwenye “Amani Yaanza Nami”

Makala: Mchoro wa Ashraf Kuku waibuka kidedea kwenye “Amani Yaanza Nami”

Pakua

Kwa wiki nne katika Chuo Kikuu cha Juba nchini Sudan Kusini, kulifanyika mashindano ya sanaa yakihusisha wanafunzi 20 kutoka chuo hicho. Maudhui yalikuwa ni Amani Yaanza Nami yakienda sambamba na miaka 75 ya operesheni za ulinzi wa amani kwenye Umoja wa Mataifa.

Mashindano hayo yaliandaliwa kwa pamoja kati ya Chuo Kikuu Juba na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani Sudan Kusini, UNMISS. Washindi watatu, kazi zao za sanaa zitawekwa kwenye lango la ofisi ya Mkuu wa Operesheni za Ulinzi wa Amani za Umoja wa Mataifa Pierre Lacroix, iliyoko makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani. Je nani aliibuka mshindi? Ungana na Assumpta Massoi kwenye makala hii. 

Audio Credit
Selina Jerobon/Assumpta Massoi
Audio Duration
4'28"
Photo Credit
Gregorio Cunha/UNMISS