Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahudumu wa afya wa vijiji Uganda wapambana na malaria kwa msaada wa UNICEF.

Wahudumu wa afya wa vijiji Uganda wapambana na malaria kwa msaada wa UNICEF.

Pakua

Malaria ni moja ya magonjwa hatari zaidi duniani ikielezwa na ripoiti ya mwaka 2022 ya shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO kuwa ilikatili maisha ya watu 619,000 duniani kote mwaka 2021 na waliougua ugonjwa huo kufikia milioni 247.

Shirika hilo linasema asilimia kubwa ya vifo na wagonjwa wako barani Afrika hasa Kusini mwa Jangwa la Sahara. Uganda ni moja ya mataifa yaliyoathirika na ugonjwa huo na wahanga wakubwa ni watoto walio na umri wa chini ya miaka mitano. Kwa kulitambua hilo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kwa kushirikiana na wadau limeanzisha program ya kuziwezesha timu za wahudumu wa afya wa vijijini VHT kushiriki katika vita dhidi ya malaria ikiwemo kwenye wilaya ya Ntungamo. Je wanafanya nini na program hiyo ina tija gani? Ungana na Selina Jerobon katika Makala hii kwa undani zaidi.

Audio Credit
Sarah Oleng'/Selina Jerobon
Audio Duration
4'9"
Photo Credit
UNICEF Video/Uganda