Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Khadija Khalid Ismail na Ebenezer Suleiman Mathew kuwawakilisha vijana wa Tanzania katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa

Khadija Khalid Ismail na Ebenezer Suleiman Mathew kuwawakilisha vijana wa Tanzania katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa

Pakua

Mwezi Septemba mwaka huu wakuu wa serikali na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kama ilivyo ada ya kila mwaka watakutana katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani kujadili masuala mbalimbali ya Ulimwengu.  

Wakati wa mkutano huu wa juu kabisa katika Diplomasia ya Umoja wa Mataifa, vijana pia hushiriki katika mikutano ya kando ili kuchangia mawazo yao katika mstakabali wa ulimwengu.  

Vijana wawili kutoka Tanzania Khadija Khalid Ismail na Ebenezer Suleiman Mathew watawakilisha vijana wenzao wakati wa Baraza hili.  

Ili kufahamu mipango yao, Stell Vuzo wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa, UNIC, jijini Dar es salaam nchini Tanzania amezungumza na mmoja wao. 

Audio Credit
Stella Vuzo na Khadija Khalid Ismail
Audio Duration
2'37"
Photo Credit
Stella Vuzo/UNIC Dar es Salaam