Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jukwaa la vijana limetukutanisha na watunga sera za mataifa mbalimbali

Jukwaa la vijana limetukutanisha na watunga sera za mataifa mbalimbali

Pakua

Tayari tangu jana Aprili 25, Jukwaa la Vijana la Baraza la Umoja wa Mataifa la Kiuchumi na Kijamii (ECOSOC) la mwaka 2023 limeng’oa nanga ambapo maelfu ya viongozi vijana kutoka duniani kote wanakusanyika katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York kujadili pamoja na mambo mengine, masuala yanayolenga kuharakisha kujikwamua kutoka janga la coronavirus">COVID-19 na utekelezaji kamili wa Ajenda ya 2030 ya Malengo ya Maendeleo Endelevu. 

Jukwaa la Vijana ndilo jukwaa kuu la vijana kuchangia mijadala ya sera katika Umoja wa Mataifa, ambapo wanaweza kutoa maoni yao, wasiwasi wao, na kuzingatia suluhu zao za kibunifu ili kukabiliana na changamoto zinazokabili ulimwengu.

Mmoja wa vijana wanaohudhuria Jukwaa hili ni Gibson Kawago anayechakata betri chakavu za kompyuta na kuzirejesha katika matumizi mengine ya uzalishaji nishati. Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa amezungumza na kijana huyu.  .

Audio Credit
Selina Jerobon/Flora Nducha
Audio Duration
3'39"
Photo Credit
UN News