Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

UNICEF/Jimmy Adriko

UNHCR yaeleza matukio ya wakimbizi na kuwatia moyo mwakani, Uganda

Mwaka 2020 umekuwa wenye changamoto nyingi zilizoathiri watu wa tabaka mbalimbali ingawa kwa viwango tofauti.

Janga la COVID-19, mafuriko katika maeneo mbalimbali na halikadhalika janga la uvamizi wa nzige katika eneo la Pembe mwa Afrika na Afrika Mashariki yalivuruga maisha kiuchumi na kijamii.

Haya yote yamekuwa na madhara hasa kwa jamii zilizohatarini wakiwemo wakimbizi.

Sauti
3'47"
UNICEF/Jimmy Adriko

Pamoja na changamoto ya COVID-19, kijana mkimbizi Uganda ajivunia mafaniko.

Licha ya mlipuko wa COVID-19 nchini Uganda kuenea hadi katika makambi ya wakimbizi ikiwemo Kyangwali na kuathiri uchumi na maisha kijamii, baadhi ya wakimbizi wamepata mafanikio na kuwa matumaini na mwaka ujao wa 2021.

Mwandishi wetu wa Uganda John Kibego amezungumza na kijana Kento Safari ambaye ni mkimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, anayejevunia mafanikio yake katika nyanja ya muziki, mipango yake mwakani na pia kuuomba Umoja wa Mataifa kuwapa msaada zaidi. 

Sauti
3'29"
UN SDGs

Vijana waendelea kushiriki katika utimizaji wa SDGs. Zauja Mohamed ni mmoja wao 

Asasi ya Nuru Yetu Foundation chini ya uongozi wa msichana Zauja Mohamed ambaye alianzisha taasisi hii akiwa katika masomo yake ya sekondari miaka michache iliyopita, hivi karibuni imeandaa warsha kwa ajili ya wasichana. Warsha hii imewakutanisha wasichana na baadhi ya watu wenye ushawishi nchini Tanzania ili wasichana hao wapate miongozo mbalimbali ya kuwasaidia kupambana na changamoto za ndani ya jamii kama vile unyanyasaji wa kijinsia, kujikwamua kiuchumi, kielimu na kadhalika.

Sauti
3'39"
FAO/Rudolf Hahn

Mabadiliko ya tabianchi, tishio kwa eneo la bonde la ufa Kenya

Kuongezeka kwa maji kwenye maziwa yaliyo eneo la bonde la ufa nchini Kenya ni jambo ambalo linaendelea kuzua wasiwasi miongoni mwa watu wa maeneo hayo na pia pigo kubwa kwa sekta muhimu ya utalii nchini Kenya. Serikali imekuwa ikiwashauri wale wanaoishi karibu na maeneo hayo kuhama na kujitafutia sehemu salama huku ikitafuta suluhusu ikiwa maji hayo yatazidi kuongezeka siku zinazokuja. Mwandishi wa Kenya Jason Nyakundi amezungumza na mtaalamu wa hali ya hewa nchini Kenya Henry Ndede kutaka kufahamu chanzo ni kipi.

Sauti
2'38"
Warren Bright/UNFPA Tanzania

Waandishi wa habari nao wapata elimu kuhusu SDGs Tanzania

Kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa UNIC Dar es Salaam kimewaelimisha waandishi wa habari wa Morogoro Tanzania kuhusu Malengo ya maendeleo endelevu. Kupitia makala hii iliyoandaliwa na Ahimidiwe Olotu, Stella Vuzo wa Kituo hicho cha habari cha Umoja wa Mataifa anaanza kwa kueleza nia ya mafunzo.

Sauti
2'57"
UN Tanzania/Ahimidiwe Olotu

Mimi nina uwezo wa kubeba mimba miezi 9, siwezi nikanza kudai mwanaume naye abebe mimba-Getrude Mongela  

Miaka mitano iliyopita, viongozi wa ulimwengu walifikia azimio kwamba, Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu, SDGs, kwa uratibu wa Umoja wa Mataifa, inabidi yawe yamefikiwa ifikapo mwaka 2030. Bi. Getrude Mongela, ambaye alikuwa Katibu Mkuu wa mkutano wa 4 wa wanawake uliofanyika Beijing China miaka 25 iliyopita, kupitia mahojiano na Stella Vuzo wa Kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa UNIC Dar es Salaam Tanzania, anaeleza kuhusu lengo namba 5, na mtazamo wake kuhusu usawa wa kijinsia.  

Sauti
3'33"
Warren Bright/UNFPA Tanzania

Mcheza kwao hutuzwa, Kalah Jeremiah

Shirika la idadi ya watu, UNFPA limewatunukia watu ambao wanapigania usawa wa kijinsi katika jamii nchini Tanzania ambapo msanii wa Hip Hop Kalah Jeremiah amekuwa miongoni mwa watu 16 waliopata tuzo hiyo. Ahimidiwe Olotu wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa UNIC Dar es Salaam amezungumza na msanii huyo. 

 

Sauti
3'10"
UN News/Yasmina Guerda

Mbao ambazo zingetupwa, nazibadili kuwa samani za nyumba

Wanawake wengi duniani, pamoja na sababu nyingine, kutokuwa huru kiuchumi kunawaweka katika hatari ya kunyanyaswa. Catherine Soi wa Kisumu Kenya, amejikwamua na hali hiyo, kwa kubadili mbao ambazo zingetupwa kama asingezibadili kuwa samani za nyumbani. Catherine Soi alitoa ujuzi wake kwenye mitandao wa intaneti na kupitia mtandao wa intaneti ndiko anapatumia sana kufanyia biashara yake. Biashara ya kutengeza fanicha au samani kutokana na mbao zinazotumika kebebea na kuhifadhi mizigo yaani pallets, kazi ambayo imemjenga kiuchumi na kumpa umaarufu wa jina jipya la pallet girl.

Sauti
2'8"

Juhudi za mwanahabari kuchagiza msaada wa kibinadamu Uganda

Kuna msemo unaosema kutoa ni moyo, usemi huu ni dhahiri kwa kuangalia mwanahabari Sophie kutoka Uganda ambaye alikuwa akitumia nafasi yake kuchagiza msaada wa kibinadamu lakini sasa anafanya kwa vitendo. Kutoka kuwa mtanganzaji na sasa ni mhudumu wa kibinadamu, basi ungana na John Kibego katika makala ifuatayo.

Sauti
3'19"