Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

UN/ Tobin Jones

Kombe la amasaza kiungo muhimu cha kuunganisha jamii Hoima Uganda

Michezo ni moja ya mbinu ambazo zinaweza kutumika katika jamii ili kuendeleza amani na uwiano katika jamii. Nchini Uganda kwa kutambua umuhimu wa michezo, wameanzisha kombe la Amasaza la eneo la ufalme wa Bunyoro. Kombe hilo la Amasaza linaleta pamoja makundi mbalimbali ya jamii na hivyo ni kiungo muhimu katika jamii wilayani Hoima. Basi ungana na John Kibego katika makala ifauatayo ikiangazia kombe hilo.

Sauti
3'24"
Diana Nambatya/Photoshare

Afya ya uzazi na ulinzi wa wanawake na wasichana ni jukumu la wote-Restless Development

Afya ya uzazi ni suala ambalo ni muhimu katika jamii yoyote, lakini upatikanaji wa huduma hii hukabiliwa na changamoto mbalimbali na hivyo kuwaweka wasichana na wanawake katika mazingira magumu. Nchini Tanzania juhudi za serikali zinasaidia kulinda wasichana na wanawake katika kupata huduma muhimu za afya ya uzazi lakini pia mashirika yasiyo ya kiserikali yanaziba pengo ambalo linasalia.

Sauti
4'1"
FAO/Luc Genot

Mafunzo ya kukabili mabadiliko ya tabianchi ni ufunguo wa kiuchumi kwa wananchi wa Madagascar

Wakati dunia ikishuhudia mwamko wa umuhimu wa kulinda na kuhifadhi mazingira kwa ajili ya kupunugza athari hasi za mabadiliko ya tabianchi, nuru imeangaza kwa wakazi wa mji wa Mangatsiotra nchini Madagascar kufuatia mradi wa kuwawezesha kukuza mazao yanayostahimili ukame na hivyo kuwa na uhakika wa chakula na pia kuongeza mapato ya wenyeji. Je nini kimefanyika? Ungana basi na Grace Kaneiya kwenye makala ha

Sauti
2'20"
UN News/Grece Kaneiya

Kundi la wasichana wakimbizi laleta burudani kwenye Umoja wa Mataifa

Mkataba wa kimataifa kuhusu wakimbizi umepitishwa rasmi wiki hii na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Licha ya kwamba mkataba huo hauna masharti ya kisheria lakini unatoa mapendekezo ya utaratibu wa kusaidia wakimbizi na nchi zinazowahifadhi pamoja na kuimarisha mazingira ya wakimbizi ili kubadili mtazamo wa kuona watu hao kama mzigo katika jamii na badala yake kukubalika kama sehemu ya jamii walikokimbilia.

Sauti
3'47"
© UNICEF/UN0188875/Njiokiktjien

Huduma za afya bado ni changamoto Burundi

Afya nzuri na maisha bora, wakati mwingine hutegemea, huduma nzuri za matibabu. Umoja wa Mataifa umesisitizia hilo katika lengo namba 3 la malengo yake  ya maendeleo endelevu, SDGs au ajenda 2030 . Hata hivyo katika baadhi ya mataifa barani Afrika hasa yale masikini, huduma hizo huwa zina walakini. Mfano,nchini Burundi katika baadhi ya maeneo bado wakazi wamekuwa wanakumbwa na  usumbufu wa kupata huduma nzuri za afya. Hii inatokea licha ya taifa hilo kutoa huduma bure za afya kwa watoto na kinamama wajawazito, bado  imekuwa ni kero kubwa kupata huduma nzuri za afya.

Sauti
4'41"
Photo: Hans Andersen

Sanaa ya uchongaji yahitaji uvumilivu:Kijana Augustino James

Wahenga walinena"mstahimilivu hula mbivu" usemi unahitajika sana katika kazi ya sanaa hususan ya uchongaji ambayo wakati mwingine huchukua siku hata miezi kabla ya kuona mafanikio yake. Kutokana na changamoto za ajira kwa vijana kote duniani wengi wameamua kuendeleza vipaji vyao vya sanaa iwe ya kuimba, kuchora na hata kuchonga vinyago kama alivyo kijana  Augustino James mkazi wa Morogoro Tanzania. Augustino anasema  sanaa ya uchongaji ni nzuri, ina toa ajira na kukidhi mahitaji lakini ina changamoto kubwa inayostahili uvumilivu ambao vijana wengi si rahisi kuukumbatia.

Sauti
3'16"
UN News

Ufahamu wa Kiswahili wamwinua mwananchi wa Uganda miongoni mwa wakimbizi

Lugha ya Kiswahili imeendelea kusambaa na kukita mizizi hata katika maeneo ambayo hapo awali haikuwa na nguvu. Na kuenea kwa lugha hiyo adhimu kunachagizwa na matukio tofauti tofauti iwe amani na hata wakati mwingine mizozo. Ni katika mazingira kama hayo ambapo mwananchi wa Uganda Nsungwa Anette Khadja ameitumia fursa ya uhitaji wa lugha ya Kiswahili katika kambi ya wakimbizi ya Kyangwali wilayani Hoima nchini humo kwa kujifunza Kiswahili na sasa anafundisha lugha hiyo kwa wanafunzi wakimbizi na wenyeji.

Sauti
3'44"
Maktaba

Mwinoghe yanoga hadi kutambuliwa na UN

Hebu fikiria ni furaha iliyoje pale utamaduni wako tena ngoma ya kijadi inapotambuliwa na Umoja wa Mataifa kuwa ni tamaduni isiyogusika na ni muhimu kiasi ya kwamba inabidi iwekwe kwenye orodha maalum. Basi furaha hiyo iliwafikia wananchi wa maeneo ya kaskazini mwa Malawi mwezi Novemba mwaka huu wakati kamati ya turathi za tamaduni zisizogusika ilipokutana huko Mauritius na kutambua ngoma moja ya kitamaduni kutoka Malawi kuwa ni miongoni mwa tamaduni hizo.

Sauti
4'25"
© UNHCR/Rose Ogola

Hatua zimepigwa lakini kuna fursa ya kulinda haki za watu wenye ulemavu Tanzania-Lihiru

Takwimu za shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO zinakadiria kuwa  takriban asilimia 80% ya watu wenye ulemavu wanaishi katika maisha ya ufukara .

Kwa mantiki hiyo unaendelea kuzichagiza nchi kote duniani  kuhakikisha watu wenye ulemavu wanasaidiwa  na kujumuishwa katika mipango yao ya maendeleo. Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazozingatia hilo kwa kupitia kupitia mikakati mbalimbali iliyoweka pamoja na utetezi wa haki za watu wanaoishi na ulemavu.

Sauti
3'25"