Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ingawa kuna changamoto najitahidi kutunza familia yangu- Tsinduka

Ingawa kuna changamoto najitahidi kutunza familia yangu- Tsinduka

Pakua

Hii leo ni siku ya kimataifa ya familia duniani ambapo maudhui ya mwaka huu ni mienendo ya makundi ya watu na familia wakati huu ambapo idadi ya watu inaongezeka ingawa kwa kiwango cha chini. Umoja wa  Mataifa unasema kupungua kwa idadi ya wanafamilia hutoa fursa ya familia kupatia huduma bora zaidi watoto, mathalani elimu na afya.

Lakini ni ndivyo sivyo kwa familia moja huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako pamoja na baba na mama kuhaha kupatia mahitaji familia yao, waasi wanaleta changamoto kwani hata mazao shambani yanavunwa na waasi badala ya kunufaisha familia. Je nini kinafanyika? George Musubao amefika kwenye kaya hiyo. 

Audio Credit
Selina Jerobon/Assumpta Massoi
Audio Duration
4'26"
Photo Credit
UN News/George Musubao