Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF Ghana yarahisisha vijana kupata huduma za afya ya uzazi na masuala ya kujamiiana 

UNICEF Ghana yarahisisha vijana kupata huduma za afya ya uzazi na masuala ya kujamiiana 

Pakua

Huduma za afya ya uzazi na masuala ya kujamiiana mara nyingi hupata vikwazo hasa pale zinapolenga vijana na barubaru. Hii ni kwa kuzingatia kuwa penginepo pahala ambapo huduma hizo zinatolewa si rafiki kwa vijana na hivyo kuhofia kufuata huduma hizo kunaweza kuwa chanzo kwa wao kubainika jambo ambalo wanadhani si jema kwao.

Ni kwa kutambua hilo, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF nchini Ghana imeibuka na mbinu mbadala inayowapatia vijana uhakika wa usalama wa taarifa zao na yale wanayotaka kufahamu ili kuwe na afya bora ya uzazi. Je ni mbinu gani hiyo? Fuatana na Assumpta Massoi kwenye makala hii iliyoandaliwa na UNICEF Ghana. 

Audio Credit
Selina Jerobon/Assumpta Massoi
Audio Duration
4'36"
Photo Credit
UNICEF/UN527200/ANNANKRA