Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN na wadau waimarisha usaidizi kwa waathirika wa mafuriko huko Kalehe, DRC

UN na wadau waimarisha usaidizi kwa waathirika wa mafuriko huko Kalehe, DRC

Pakua

Ni takribani wiki moja tangu eneo la Kalehe lililoko jimbo la Kivu Kusini nchini DRC, likumbwe na mafuriko kufuatia kuongezeka kwa kina cha maji katika mito kulikosababishwa na mvua kubwa.  Serikali ya DRC na mashirika yasiyo ya kiserikali yametuma wajumbe mbalimbali papo hapo kwenda kufanya uchunguzi ili kutoa misaada ya kibinadamu kwa wahanga.  

Mwandishi wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa nchini DRC George Musubao amezungumza kwa njia ya simu na Yvon Edoumou ambaye ni msemaji wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya uratibu wa misaada ya dharura,  OCHA nchini humo ili kufahamu hali inaendeleaje. 

Audio Credit
Selina Jerobon/Assumpta Massoi
Audio Duration
3'55"
Photo Credit
© WFP