Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

​​​​​​​Nafasi yangu kama mama, mwanamke na mke wa Rais imenisukuma kuisaidia jamii yangu: Mariam Mwinyi

​​​​​​​Nafasi yangu kama mama, mwanamke na mke wa Rais imenisukuma kuisaidia jamii yangu: Mariam Mwinyi

Pakua

Wakati macho . masikio na nguvu za dunia zikielekezwa katika utimizaji wa malengo ya maendeleo endelevu SDG’s yanayofikia ukomo mwaka 2030, kila nchi inafanya jitihada za hali na mali kuhakikisha jamii inafikia malengo hayo. 

Na visiwa vya Zanzibar nchini Tanzania havijasalia nyuma, serikali na wanahatrakati mbalimbali wamelivalia njuga suala hilo wakitumia kila mbinu ili kusongezha hatua za kutimiza malengo hayo. Miongoni mwa wanaharakati hao ni mke wa Rais wa visiwa hivyo Bi. Mariam Mwinyi ambaye mwishoni mwa wiki amezindua wakfu au taasisi maalum ya “Zanzibar Maisha bora kwa wote foundation”. Je anajikitina na nini hasa? Na nini kimemsukuma kuanzisha wakfu huo sasa? Ungana na Flora Nducha na Bi Mariam katika mahojiano haya 

(MAHOJIANO NA MARIAM MWINYI) 

Audio Credit
Flora Nducha/ Mariam Mwinyi
Audio Duration
10'15"
Photo Credit
Ikulu Zanzibar