Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maji ni zawadi toka kwa mungu hivyo ni haki ya kila mtu: Fr. Benedict Ayodi

Maji ni zawadi toka kwa mungu hivyo ni haki ya kila mtu: Fr. Benedict Ayodi

Pakua

Mkutano wa maji wa Umoja wa Mataifa unaanza leo Machi 22 hapa makao makuu ukibeba maudhui hatua za ajenda ya kuhakikisha upatikanaji wa maji kwa wote, kwani hatua hizo za maji zinaongeza uhakika wa chakula, usawa miongoni mwa jinsia, zinahakikisha watoto wanasalia shuleni, zinafanya jamii kuishi kwa amani na kuchangia mazingira yenye afya.

Umoja wa Mataifa unamtaka kila mtu kuchukua hatua na sasa na shirika la kimataifa lisilo la kiserikalia la Wakapuchini wa Fraciscan ni miongoni mwa wanaochukua hatua hizo ili kuhakikisha rasilimali hii muhimu inamfikia kila mtu.

Kufahamu zaidi kuhusu shirika hilo na wanachokifanya Flora Nducha amemezungumza na Fr Benedict Ayodi wa shirika hilo ambaye anaanza kwa kueleza kuhusu shirika lao

 

Audio Credit
UN News/Flora Nducha
Audio Duration
7'17"
Photo Credit
UN News