Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kazi ya ulinzi wa amani UM ni zaidi ya kubeba mtutu wa bunduki

Kazi ya ulinzi wa amani UM ni zaidi ya kubeba mtutu wa bunduki

Pakua

Kikosi kazi cha nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa wanaochangia vikosi vya kulinda amani kimekuwa kikikutana hapa makao makuu tangu Januari 16 na mkutano wao umehitimishwa leo Ijumaa.

Kikosi hicho kimekuwa kikijadili masuala mbalimbali yanayohusiana na uchangiaji wa vikosi, vifaa, afya na jinsi ya kuboresha huduma kwa nchi wanachama.

Ili kupata undani wa kilichojiri mkutanoni Flora Nducha ameketi na Meja jenerali mstaafu Paul Meela na Meja Jenerali Issa Narsorro walioiwakilisha Tanzania kwenye kikao hicho. Kwanza Meja jenerali Meela anaelezea kuhusu mada zilizotamalaki.

(MAHOJIANO NA MEELA NA NASORRO)

Photo Credit
Wakati wa mahaojiano kati ya Flora Nducha wa Idhaa hii, Luteni jenerali mstaafu Paul Mella na Meja Jenerali Issa Narsorro .(Picha:UM/Assumpta Massoi)