Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

Kuelekea 2030, wanawake wamejizatiti kufikia #5050

Tarehe Nane mwezi Machi, kwa zaidi ya karne moja sasa, imekuwa ni siku  ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani. Siku hii ikiangazia harakati za kuweka usawa wa kijinsia kwa mustakhbali bora siyo tu wa kundi hilo ambalo ni zaidi ya asilimia 50 duniani, bali pia kwa ulimwengu wote kwani wahenga walisema ukimwendeleza mwanamke umeendeleza jamii nzima.

Sasa katika maadhimisho haya tumetathmini hali ya mwanamke kiuchumi, kisiasa na kijamii na mwelekeo wa usawa wa 50 kwa 50 ifikapo mwaka 2030 katika mazingira ya sasa ya kazi ulimwenguni yanayobadilika.

Tukipata teknolojia wezeshi tutazalisha maradufu: Wajasiriamali Wanawake

Ukosefu wa teknolojia wezeshi unapunguza mapato kusudiwa kwa wanawake mkoani Kagera nchini Tanzania, hii ni kwa mujibu wa wajasiriamali mkoani humo ambao wanasema wakiwezeshwa kiteknolojia watazalisha maradufu.

Nicolaus Ngaiza wa redio washirika Kasibante Fm ya Kagera nchini humo, amevinjari hadi wajasiriamali hao wanawake wanapofanya kazi zao ili kujionea. Ungana naye katika makala ifuatayo.

Kutana na Adian Coker, mwanamuziki anayekataa ubaguzi

Burudani na ujumbe! Ndivyo unavyoweza kusema ukitafakari ushairi wenye vina unaeleta hisia za ujumbe kuhusu kupinga ubaguzi wa kila aina.

Huu ni ujumbe wa mwanamuziki Adina Coker mkazi wa Uingereza ambaye ameamua kuingia vitani dhidi ya ubaguzi sambamba na Umoja wa Mataifa unaopinga dhana hiyo.Ungana na Assumpta Massoi katika midundo hiyo.

Bila elimu bure sisi tusingesoma-Wasichana Uganda

Katika kutimiza lendo namba nne la maendeleo endelevu SDGs, linalotaka uwepo wa usawa katika elimu, Uganda imepiga hatua kwa kuhakikisha elimu bure hatua iliyowezesha wale wasiojiweza kwenda shule.

Ungana na John Kibego ambaye amefuatailia upatikanaji wa elimu nchini humo ambapo pia amezungumza na wanufaika wa mpango huo.

Juhudi za kuinua elimu kwa mtoto wa kike Uganda

Lengo namba la nne la maendeleo endelevu SDGs, linaangazia usawa wa kielimu, likipigia fursa kwa makundi yote hususani jinsia. Kwa kuzingatia hilo jumuiya ya kimataifa inawajibika kutekeleza lengo hilo ili kukuza kiwango cha elimu.

Nchini Uganda, dhana ya kumuelimisha mtoto wa kike inashika kasi, kama anavyosimulia John Kibego katika makala ifuatayo.

Redio imerahisisha mawasiliano miongoni mwetu: Wakimbizi

Wakimbizi wawapo kambini huendelea na maisha kama jamii nyingine, hivyo huhitaji mawasiliano ya mtu na mtu na makundi mengine ya kijamii. Mchakato wa mawasiliano hukabiliwa na vikwazo kama vile kuchelewa kwa ujumbe au kutofika kabisa. Ndiposa redio kama chombo cha habari hutumika kuwafikishia taarifa tofautitofauti na kuwaelimisha kuhusu mambo yawahusuyo.

Katika mfululizo wa makala leo tunamulika umuhimu wa redio kwa wakimbizi walioko Kigoma Tanzania, ambapo Kongolo Mubanga Kahenga wa redio washirika redio Umoja ya Kigoma Tanzania anazungumza na kundi hili.

Radio kama chemchemi ya burudani

Wakati radio inatajwa kuwa chombo muhimu katika baadhi ya mambo ikiwemo burudani katika jamii mara nyingi watu huwazia tu msikilizaji anayepata kuburudika kupitia radio lakini, kwa upande mwingine ni wanamuziki ambao wanategemea radio katika kupitisha ujumbe wao kwa mfumo wa nyimbo. Je radio ina mchango gani kwa wanamuziki hususan katika nchi zinazoendelea?

Basi Ungana na Geoffrey Onditi wa radio washirika Shirika la utangazaji nchini Kenya, KBC

Wasikilizaji Vindakindaki watoa ya moyoni kuhusu umuhimu wa redio

Juma hili dunia ikiwa imeadhimisha siku ya redio mnamo Februari 13, wasikilizaji hususani wale wanaotufuatilia kupitia tovuti mathalani Facebook, wamesema uwepo wa idhaa hii ni muhimu kwa kuwapasha habari za kitaifa na kimataifa , huku wengine wakitoa maoni yao juu ya nini cha kuboreshwa.

Wasikilizaji hao ambao walitoa namba zao ili kuzungumza na kueleza hisia zao katika kuadhimisha siku ya redio duniani, maoni yao yamejikita zaidi katika namna wanavyonufaika na redio kwa ujumla na kisha idhaa ya Kiswahili ya redio ya Umoja wa Mataifa.

( SAUTI ZA WASIKILIZAJI)