Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tatizo la msongo wa mawazo na athari za afya ya akili

Tatizo la msongo wa mawazo na athari za afya ya akili

Pakua

Kwa mujibu wa shirika la afya ulimwenguni WHO, msongo wa mawazo ambao ni mvurugano katika akili hutokana sababu kadhaa kama vile mkwamo katika uhusiano, uchumi na mengineyo, huwakumba mtu mmoja kati ya wanne kwa nyakati tofauti.

Kwa takribani watu milioni 350 duniani wameathiriwa na msongo wa mawazo. WHO inasema, unyanyapaa dhidi ya wagonjwa, huzuia watu wengi kutafuta msaada.

Kama hiyo haitoshi, zaidi ya asilimia 75 ya watu wanaokabiliwa na ugonjwa huu katika nchi zinazoendelea  hawapati matibabu.

Cha kusikitisha zaidi msongo wa mawazo ni chanzo namba mbili kwa vifo vya vijana wenye umri kati ya miaka 19 hadi 29.

Photo Credit
Mgonjwa katika hospitali ya watu wenye matatizo ya afya ya akili mjini Kabul.(Picha:UM/Eskinder Debebe)