AMISOM watoa mafunzo ya kuukabili ukatili wa kingono na kijinsia Somalia.

AMISOM watoa mafunzo ya kuukabili ukatili wa kingono na kijinsia Somalia.

Pakua

Ripoti kadhaa za haki za binadamu barani Afrika, zinaitaja Somalia kama moja ya nchi ambazo ukatili wa kijinsia na kingono hutendeka kwa wingi na kutaka hatua zichukuliwe.

Katika kuhakikisha hilo, ujumbe wa Muungano wa Afrika nchini humo AMISOM, unatoa mafunzo kwa maafisa wa polisi na jamii juu ya namna ya kukabiliana na ukatili huo. Assumpta Massoi anakupasha kwa undani katika makala ifuatayo.

Photo Credit
Mafunzo ya kuukabili ukatili wa kingono na kijinsia Somalia. Picha: UM/Video capture