Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Familia na makuzi yake hususan nchini Uganda

Familia na makuzi yake hususan nchini Uganda

Pakua

Familia!  Msingi bora wa jamii na taifa kwa ujumla.Kuna usemi usemao, Taifa bora hujengwa na familia bora. Kwa kutambua hilo, Umoja wa Mataifa unaenzi familia kwa kuadhimisha siku ya duniani kila tarehe 15 ya mwezi Mei. Mwaka huu ujumbe ni Familia, elimu na ustawi.

Maadhimisho yanalenga katika jukumu la taasisi hiyo na sera za kukuza elimu na kwa ujumla ustawi wa familia. Kwa ujumla siku hii inajikita katika kuelimisha familia katika kukuza elimu utotoni pamoja na fursa za muda mrefui kwa mtoto na kijana.

Umoja wa Mataifa katika ujumbe wake kwa mwaka huu unasistiza umuhimu wa watu wanaojali familia mathalani wazazi ,babu na bibi, au kaka na dada katika elimu ya maelezi kwa watoto.

Ujumbe unaenda mbali zaidi kwa kumulika matendo mema wayafanyao walezi katika usaidizi kwa wazazi huku wakiweka urari kwenye kutoa elimu  kwa watoto. Kadhalika jukumu la sekta bianafsi kusaidia walezi na vijana kwa kazi hiyo.

Na katika kupambanua ujumbe huo mwandishi wetu nchini Uganda, John Kibego amevinjari kuangalia wajibu wa familia na sekta mbalimbali ikiwemo ile ya kibinafsi katika ujenzi wa familia.

Photo Credit
Muundo wa familia hii ni baba, mama na mtoto.(Picha:UNFPA)