Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msichana wa Kisomali aonyesha jinsi azma na uthabiti inavyoweza kubadili maisha

Msichana wa Kisomali aonyesha jinsi azma na uthabiti inavyoweza kubadili maisha

Pakua

Iqra Ali Omar, msichana mwenye umri wa miaka 19, alianza kuishi na jamaa zake, wazazi wake walipoachana akiwa mtoto mdogo sana.

Isingalikuwa kwa ajili ya moyo wake thabiti, hatma yake ingalikuwa kama ya wasichana wengine wengi wa Kisomali, ambao kawaida hulazimishwa na familia zao maskini kuingia ndoa za utotoni.

Baada ya serikali ya kitaifa ya Somalia kusambaratika mnamo mwaka 1991, jukumu la Wizara ya Elimu lilichukuliwa na taasisi za kibinafsi, ambazo zilisajili na kutoa huduma za elimu ya malipo kwa watoto wenye umri wa kwenda shule.

Watoto ambao wazazi wao walikuwa hawawezi kumudu kulipa karo ya shule, walikaa nyumbani, bila huduma ya elimu, Iqra akiwa mmoja wao. Kupata mengi zaidi kuhusu hatma ya Iqra, ungana na Joshua Mmali katika makala ifuatayo

Photo Credit
Iqra Ali Omar.(Picha:UNIfeed/Video Capture)