Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Natamani wasio walemavu wavae viatu vyetu: Mwakilishi walemavu Tanzania

Natamani wasio walemavu wavae viatu vyetu: Mwakilishi walemavu Tanzania

Pakua

Kila anayetunyima fursa tunatamani angevaa viatu vyetu, ahisi uchungu tunaopitia, ni kauli ya mmoja wa wawakilishi wa watu wenye ulemavu kutoka Tanzania Zanzibar Bi Abeida Rashid Abdallah, Mkurugenzi Idara ya Watu wenye ulemavu kwenye ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.

Bi Abeida anyehudhuria mkutano wa 10 wa nchi wanachama wa mkataba wa watu wenye ulemavu CRPD, unaomalizika juma hili mjiniNew York, amemweleza Joseph Msami katika mahojiano maalum kwamba wanachokihitaji ni kuona mkataba huo ambao Tanzania imeridhia unatakelezwa.

Photo Credit
Bi Abeida Rashid Abdallah, Mkurugenzi Idara ya Watu wenye ulemavu kwenye ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar. Picha: UM/Idhaa ya Kiswahili