Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dunia itupie macho visiwa vya Afrika kulinda bahari: Dk Tizeba

Dunia itupie macho visiwa vya Afrika kulinda bahari: Dk Tizeba

Pakua

Macho yote yameelekezwa kwenye visiwa vya Magharibi, hili lapaswa kukoma! Ni kauli ya Waziri wa kilimo, mifugo na uvuvi wa Tanzania Dk Charles Tizeba wakati akihutubia mkutano wa kimataifa kuhusu bahari unaoendelea mjini New York.

Katika mahojiano maalum na Joseph Msami wa idhaa hii, Dk Tizeba ameitaka jumuiya ya kimataifa kutozisahau nchi zinazoendelea zenye visiwa ambazo zaweza kunufaika kiuchumi na kijamii na uwepo wa bahari.

Hata hivyo amesema anatiwa moyo kwamba nchi zilizoendelea zinajali mustakabali wa bahari. Kwanza Waziri Tizeba anaanza kwa kuelelezea kilio cha serikali ya Tanzania.

Photo Credit
Waziri wa kilimo, mifugo na uvuvi wa Tanzania Dk Charles Tizeba.Picha: UM/Idhaa ya Kiswahili