UNAMID yasaidia kuzima moto Korma, Darfur

UNAMID yasaidia kuzima moto Korma, Darfur

Pakua

Nchini Sudan katika jimbo la Darfur, walinda amani wa ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika, UNAMID waliwezesha kuepusha janga zaidi baada ya kushiriki kuzima moto katika kijiji cha Korma.

Hivi sasa wakazi wa eneo hilo kwa usaidizi wa UNAMID wanajaribu kurejea katika maisha ya kawaida baada ya kunusurika na zahma hiyo. Je nini kilitokea? Jumbe Omari Jumbe wa radio ya ujumbe huo wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika, UNAMID anasimulia kwenye makala hii.

Photo Credit
Moto katika kambi ya wakimbizi wa ndani ya Korma yateketeza makazi ya wenyeji.(Picha: Lokraj Yogi, UNAMID.)