Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

Wakimbizi wa CAR wakimbilia nchi ya DRC

Huku kukiwa na taarifa za kuendelea kwa mapigano ndani ya Jamhuri ya Afrika ya Kati ,katika mji mkuu Bangui maelfu ya raia wa nchi hiyo wanakimbia ili kutafuta hifadhi na...................... kwa sasa wamekuwa wakivuka mto uitwao Oubangui na kutafuta makazi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na katika jimbo la Orientale. Joseph Msami ameandaa taarifa ifuatayo.

Hali ya usalama yarejea Mogadishu: Mahiga

Hali ya usalama imeripotiwa kurejea mjiniMogadishu, nchiniSomalia, siku tatu baada ya mashambulizi ya kushtukiza mjini humo yaliyosababisha vifo vya makumi kadhaa ya watu na wengine kujeruhiwa. Taarifa hizo ni kwa mujibu wa Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, Balozi Augustine Mahiga ambaye katika mahojiano maalum na Grece Kaneiya wa Idhaa ya Kiswahili ya Radio ya Umoja wa Mataifa amesema hali ya usalama inaendelea kuimarika na ulinzi utaimarishwa bila kuwanyima wananchi haki yao ya kufuatilia masuala ya haki.

Mahitaji yameongezeka nchini Chad:IOM

Shirika la Kimataifa la Uhamiaji, IOM limesema idadi kubwa ya wahamiaji na wakimbizi wanaomiminika nchini Chad wamesababisha ongezeko la mahitaji ya kibinadamu ambayo nchi hiyo hiyo pekee haiwezi kutosheleza, na hivyo kuomba ufadhili wa haraka ili kuwanusuru.

Katika mahojianao na Grace Kaneiya mseaji wa IOM Jumbe Omari jumbe anasema dola milioni tatu na nusu zinahitajika kwa dharura kuwasaidia wakimbizi na wahamiaji hao, ambao wengi wanatoka nchini Sudan, Libya na wengine Jamhuri ya Afrika ya kati.

(MAHOJIANO- JUMBE)

Adha za wakimbizi wa Syria zamulikwa

Wakuu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, jana kwa pamoja wamezipazia sauti pande zote katika mzozo wa Syria na serikali zenye ushawishi zifanye kila ziwezalo kuwaokoa watu wa Syria kutokana na watu wa Syria na ukanda mzima kutokana na baa la vita. Licha ya kuanisha msaada badounahitajika lakini wamesisitiza pande zinazozozana kuyaacaha mapigano hima.

Ungana na Joseph Msami anayengazia hali mbaya za wakimbizi wa Syria waliojko nchini Uturuki wakitafuta hifadhi

Mashambulio mjini Mogadishu hayatukatishi tamaa: Balozi Mahiga

Siku ya Jumapili ilikuwa ya giza nene hukoMogadishu,Somalia baada ya kuwepo kwa mfululizo wa mashambulio ya mabomu wakati huu ambapo serikali ya nchi hiyo inaendelea kushirikiana na wadau mbali mbali kuimarisha usalama ili shughuli za maendeleo ziweze kufanyika. Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Balozi Augustine Mahiga alizungumza na Joseph Msami wa Radio ya Umoja wa Mataifa ambapo pamoja na kulaani shambuliohilona kusema kuwa licha ya kuleta madhara makubwa haliwakatishi tamaa katika kutafuta amani ya kudumu hukoSomalia.

Wahamiaji wa Tawerika Libya wapata afueni kwa msaada wa IOM

Miaka miwili bada ya mapigano yalioikumba Libya, baadhi ya raia wa nchi hiyo, wamegeuka wahamiaji katika nchi yao kutokana na chuki za kisiasa. Mathalani jamii ya Tawerika yenye idadi ya takribani watu 30, 000 ambao wamesambaa sehemu kadhaa za mjini Tripoli na sehemu nyingine  kutafuta makazi.

Kufuatia hilo Shirika la kimataifa la Uhamiaji IOM likishirikiana na asasi 37 za kiraia limeanza kugawa misaada isiyo ya chakula nchini Libya ili kunusuru maisha ya wahamaji hao wa ndani .

Uhifadhi wa misitu kuchochea utalii Kenya: Kabugi

Huko Istanbul, Uturuki mkutano wa kimataifa kuhusu mustakhbali wa misitu duniani unaendela na kubwa ni jinsi gani misitu inaweza kusaidia kuchochea maendeleo ya kiuchumi. Donn Bob wa Radio ya Umoja wa Mataifa aliyeko mjini humo aliratibu mahojiano na Hison Kabugi, Mkurugenzi wa Misitu na  Wanyamapori kutoka Kenya, mahojiano ambayo yaliendeshwa nami Joshua Mmali kutoka hapa New York. Kwa kuanzia Bwana Kabugi anaelezea umuhimu wa mkutano huo wa wiki mbili kwa Kenya.

Wanawake wa ukanda, Sahel, wakutana Ubelgiji

Wanawake wa ukanda wa Sahel wamekutana mjini Brussels Ubelgiji katika kongamano la kujadili maswala ya kiuchumi na ushiriki wao katika siasa.

Mkutano huu ni hatua ya kwanza ya kuhakikisha kuwa sauti za wanawake kutoka eneo la Sahel zinasikika na kuwa maoni yao yanatiliwa maanani.

Ungana na Joseph Msami katika ripoti hii ufahamu kwa undani matumaini ya mkutano huu unaofanyika takribani mwezi mmoja tangu dunia ilipoadhimisha siku ya wanawake.

Umoja wa Mataifa kukumbuka mauaji ya kimbari Rwanda

Leo ni siku ilotengwa na Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kumbulumbu ya mauaji ya kimbari yalotokea miaka 19 iliyopita nchini Rwanda. Watu wapatao laki nane waliuawa nchini Rwanda katika kipindi cha siku mia moja mnamo mwaka 1994 nchini Rwanda.

Katika kuadhimisha siku hii, Umoja wa Mataifa na watu kote duniani hufanya hafla maalum zinazojumuisha kuwasha mishumaa na kuwa kimya kwa dakika moja ili kuwaenzi wahanga wa mauaji hayo. Hapa mjini New York, Umoja wa Mataifa utaikumbuka siku hiyo kwa hafla maalum mnamo tarehe 9 Aprili.