Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida la Habari

21 SEPTEMBA 2022

Katika Jarida la habari za Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea 

-Kandoni mwa mjadala wa wazi wa Umoja wa Mataifa shirika la afya duniani WHO limewataka viongozi wa dunia kuchukua hatua haraka kukabiliana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza NCDs yanayokatili maisha ya watu milioni 50 kila mwaka

-Kijana Mtanzania Gibson Kawago ni miongoni mwa vijana 17 waliotangazwa leo na Umoja wa Mataifa kuwa viongozi vijana wa kusongesha malengo ya maendeleo endelevu SDG's je amepokeaje uteuzi huo na anapanga kufanya nini?

Audio Duration
13'15"

19 SEPTEMBA 2022

Hii leo kwenye Habari za UN, Flora Nducha anaanza na Kauli ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu elimu, akisema elimu ndio kitu ambacho kinaweza kuleta amani na maendeleo ya kudumu duniani. Kisha ni taarifa ya mahojiano na mchechemu wa vijana wa UNICEF nchini Tanzania, Emmanuel Msoka akisema “maneno ni rahisi lakini vitendo ni aghali,” hivyo vitendo vyahitajika ili kusongesha maendeleo ya kweli. Anapendekeza kurejeshwa kwa Baraza la Vijana nchini Tanzania.

Sauti
12'4"

16 SEPTEMBA 2022

Katika Habari za UN hii leo Leah Mushi anaanzia makao makuu ya  Umoja wa Mataifa ambako kumeanza mkutano wa marekebisho ya mfumo wa elimu na kikubwa leo ni uzinduzi wa darása la mfano linaloonesha kuwa ni mtoto 1 kati ya 3 wenye umri wa miaka 10 duniani kote ndiye anayeweza kusoma na kuelewa hadithi fupi, kulikoni basi? Sababu ni mgogoro kwenye sekta ya elimu!

Sauti
11'54"

15 SEPTEMBA 2022

Hii leo katika Habari za UN ni mada kwa kina na Flora Nducha anakupeleka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako Umoja wa Mataifa umewezesha vijana sasa kuweza kujihudumia kupitia mafunzo ya kutengeneza simu janja. Msichana Sintyashi Kyaula anaeleza hali ilivyokubwa kabla ya mafunzo na baada ya mafunzo, akiwa kwenye kioski chake cha kutengeneza simu kwenye kitongoji cha Majengo, Goma, mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini.

Sauti
10'45"

14 SEPTEMBA 2022

Hii leo katika Habari za UN, Flora Nducha anaanzia na masuala ya elimu, hususan kwa kuzingatia kuwa mkutano wa ngazi ya juu wa viongozi kuhusu marekebisho ya mfumo wa elimu duniani unaanza Ijumaa hii kwenye makao makuu ya UN, New York, Marekani. Suala la watoto wa kike kuenguliwa kwenye hisabati kutokana na kukoseshwa fursa. Halikadhalika suala la haki ya elimu kupaswa kupiganiwa hivi sasa kwa kuwa elimu wanayopata watoto wengi duniani haikidhi mahitaji ya dunia hivi sasa.

Sauti
12'15"

13 SEPTEMBA 2022

Leo katika Habari za UN ni Mada kwa kina tukikupeleka Vanga Kaunti ya Kwale nchini Kenya ambako kwa miaka nenda miaka rudi sanaa imekuwa ikitumika kuhamasisha masuala mbalimbali yahusuyo jamii hiyo ambayo ni ya wavuvi. 
Mashinani tunasikia kauli ya Rais wa Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ,UNGA77 unaoanza rasmi hii leo. Je amepana kufanya nini?

Sauti
11'11"

12 SEPTEMBA 2022

Hii leo jaridani Flora Nducha anaanza kwa taarifa ya kwamba utumwa wa kisasa una aina mbalimbali ikiwemo kwenye ajira na pia kwenye ndoa. Kisha anakupeleka kaunti ya Tukrana nchini Kenya ambako UNICEF imenusuru wanawake na mwendo mrefu wa kusaka maji kwa kuwajengea mabwawa ya mchanga. Makala anakukutanisha na Hamad Rashid wa redio washirika MVIWATA FM mkoani Morogoro akikuletea mradi wa UNCDF ambao umekwamua maisha ya wakazi wa Kibondo mkoani Kigoma Tanzania kupitia ushirika wa kilimo uitwao Kibondo Big Power Group.

Sauti
11'48"

09 SEPTEMBA 2022

Katika Jarida la habari la Umoja wa Mataifa leo Ijumaa Flora Nducha anakuletea

-Katika siku ya kimataifa ya kulinda shule dhidi ya mashambulizi mashirika ya Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na la elimu sayansi na utamaduni UNESCO yanasema Afrika ya Kati na Magharibi ni nyumbani kwa karibu robo ya watoto wote duniani wasiokwenda shule  

Sauti
10'59"

08 SEPTEMBA 2022

Katika jarida la mada kwa kina hii leo kutoka Umoja wa Mataifa, Flora Nducha anakuletea 

-Ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa Maendeleo UNDP kuhusu maendeleo ya binadamu inaonyesha kuwa maendeleo hayo ya binadamu ynashuka kwa karibu asilimia 90 ya nchi duniani

Sauti
13'15"

07 SEPTEMBA 2022

Katika jarida la Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea 

-Katibu Mkuu UN atoa wito kwa ushirikiano wa kimataifa kukabiliana na uchafuzi wa hali ya hewa katika siku ya kimataifa ya hewa safi kwa ajili ya anga ya bluu

-Hatuwezi kusubiri hadi baa la njaa litangazwe Somalia tunafanya kila tuwezalo kuwanusuru Wasomali limesema shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP 

Sauti
12'18"