Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

12 SEPTEMBA 2022

12 SEPTEMBA 2022

Pakua

Hii leo jaridani Flora Nducha anaanza kwa taarifa ya kwamba utumwa wa kisasa una aina mbalimbali ikiwemo kwenye ajira na pia kwenye ndoa. Kisha anakupeleka kaunti ya Tukrana nchini Kenya ambako UNICEF imenusuru wanawake na mwendo mrefu wa kusaka maji kwa kuwajengea mabwawa ya mchanga. Makala anakukutanisha na Hamad Rashid wa redio washirika MVIWATA FM mkoani Morogoro akikuletea mradi wa UNCDF ambao umekwamua maisha ya wakazi wa Kibondo mkoani Kigoma Tanzania kupitia ushirika wa kilimo uitwao Kibondo Big Power Group. Mashinani ni kauli ya Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Profesa Kennedy Gastorn kuhusu kifo cha Malkia wa Uingereza na ushirikiano wa kimataifa. Karibu!

Audio Credit
FLORA NDUCHA
Audio Duration
11'48"