Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

16 SEPTEMBA 2022

16 SEPTEMBA 2022

Pakua

Katika Habari za UN hii leo Leah Mushi anaanzia makao makuu ya  Umoja wa Mataifa ambako kumeanza mkutano wa marekebisho ya mfumo wa elimu na kikubwa leo ni uzinduzi wa darása la mfano linaloonesha kuwa ni mtoto 1 kati ya 3 wenye umri wa miaka 10 duniani kote ndiye anayeweza kusoma na kuelewa hadithi fupi, kulikoni basi? Sababu ni mgogoro kwenye sekta ya elimu! Kisha ni Geneva, Uswisi kumulika hatua za Tanzania katika kusongesha haki za binadamu, anayezungumza ni Profesa Eliamani Sedoyeka, Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii ambaye anashiriki mkutano wa 51 wa Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za binadamu. Makala tunabisha hodi Kenya na mashinani ni kauli ya mtoto kutoka jimboni Katsina nchini Nigeria kuhusu jinsi fedha taslimu kutoka UNICEF zimemwezesha kurejea shuleni na sasa ana ndoto ya kuwa daktari.

Audio Credit
LEAH MUSHI
Audio Duration
11'54"