Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

08 SEPTEMBA 2022

08 SEPTEMBA 2022

Pakua

Katika jarida la mada kwa kina hii leo kutoka Umoja wa Mataifa, Flora Nducha anakuletea 

-Ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa Maendeleo UNDP kuhusu maendeleo ya binadamu inaonyesha kuwa maendeleo hayo ya binadamu ynashuka kwa karibu asilimia 90 ya nchi duniani

-Shirika la Umoja wa Mataifa la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO kupitiaripoti yake mpya iliyotolewa leo limesema changamoto ya maji na hatari nyingine kama vile ukame usioisha na mafuriko makubwa vinaathiri sana jamii za Kiafrika, uchumi na mifumo ya ikolojia, huku mifumo ya mvua ikitatizika, barafu inatoweka na maziwa muhimu yanapungua kina cha maji.

-Kwa mujibu wa takwimu mpya za shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM zilizotolewa leo, wanawake na wasichana ndio idadi kubwa ya wahamiaji Mashariki na Pembe ya Afrika .

-Mada kwa kina leo inajikita na mshindi wa tuzo ya polisi wa mwaka mwanamke wa Umoja wa Mataifa ambaye ni raia ya Burkina Faso anayehudumu kwenye mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Mali MINUSMA.

-Na katika kujifunza Kiswahili tuko kwenye baraza la Kiswahili la taifa Tanzania BAKIZA kupata ufafanuzi wa neno MUHARARA

Audio Credit
UN News/Flora Nducha
Sauti
13'15"