Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

14 SEPTEMBA 2022

14 SEPTEMBA 2022

Pakua

Hii leo katika Habari za UN, Flora Nducha anaanzia na masuala ya elimu, hususan kwa kuzingatia kuwa mkutano wa ngazi ya juu wa viongozi kuhusu marekebisho ya mfumo wa elimu duniani unaanza Ijumaa hii kwenye makao makuu ya UN, New York, Marekani. Suala la watoto wa kike kuenguliwa kwenye hisabati kutokana na kukoseshwa fursa. Halikadhalika suala la haki ya elimu kupaswa kupiganiwa hivi sasa kwa kuwa elimu wanayopata watoto wengi duniani haikidhi mahitaji ya dunia hivi sasa. Makala tunakwenda katikati mwa Tanzania, wilayani Ikungi katika mkoa wa Singida ambako mradi wa umeme wa nishati ya jua kupitia ufadhili wa shirika la mitaji la Umoja wa Mataifa, UNCDF umeanza kuzaa matunda kwa wananchi. Anatamatisha na mashinani na anakupeleka nchini Afghanistan kusikia changamoto za elimu kwa wasichana zilizoletwa na utawala wa Taliban. Karibu!

Audio Credit
FLORA NDUCHA
Audio Duration
12'15"