Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

UNEP yazingatia hifadhi ya mikoko katika Bahari ya Pasifiki.

Shirika la UNEP limetangaza kwamba utafiti ulioendelezwa karibuni kuhusu hali ya mikoko katika Bahari ya Pasifiki umethibitisha ya kuwa kunahitajika kuchukuliwa hatua za haraka za pamoja, kimataifa, kuhifadhi uchumi wa mfumo muhimu wa ikolojia ya eneo hilo. Mabadiliko ya hali ya hewa yalionekana kukithirisha kima cha usawa wa bahari na kuhatarisha mazingira maumbile ya eneo.

Mtaalamu wa UM athibitisha uchumi maendeleo umeshindwa kuzalisha ajira.

Charles Gore, Mtaalamu aliyetayarisha Ripoti ya UM ya 2006 juu ya Maendeleo ya Mataifa Yanayoendelea (LDC) amearifu wiki hii kwamba ijapokuwa katika 2004 maendeleo ya uchumi katika nchi masikini yaliongezeka kwa kiwango cha 5.9, muongezeko huu ulishindwa kupanua fursa za ajira na pia kutofanikiwa kupunguza ufukara na hali duni, kwa ujumla, katika maeneo hayo.

Wanajeshi walinzi wa UM waachiwa huru nchini Congo-DRC.

Wanajeshi watano walinzi wa amani wa UM kutoka Nepal waliotekwa nyara na kundi la waasi la FNI katika JKK kuanzia tarehe 28 Mei (2006) waliachiwa huru majuzi wakiwa na afya zao imara. Wanajeshi hawa hivi sasa wameshajiunga na vikosi vya kuimarisha amani vya UM ili kujiandaa na kusimamia hali ya utulivu ndani ya nchi kabla ya uchaguzi mkuu wa taifa mwisho wa mwezi.~~

Ripoti ya KM kuhusu mzozo nchini Uganda Kaskazini.

Ripoti ya KM iliyowasilishwa karibuni kuhusu mzozo wa Uganda ya Kaskazini imesisitiza ya kuwa licha ya Serekali za mataifa jirani kujaaliwa uwezo na dhamana ya kukabiliana na utenguzi wa haki za kiutu unaoendelezwa na kundi la waasi la LRA dhidi ya raia, kwa wao kuweza kulidhibiti tatizo hilo kithabiti na kusawazisha usalama wa eneo, watahitajia vile vile msaada na ujuzi wa UM.~~