Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Mwakilishi wa KM kwa Usomali apendekeza ujumbe wa kurudisha amani

Mwakilishi Maalumu wa KM kwa Usomali, Francois Lonseny Fall wiki hii amemtumia Sheikh Sharif Sheikh Ahmed, Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Kundi la Mahakama za Kiislamu mjini Mogadishu barua inawayohimiza kupeleka wawakilishi wao kwenye duru ya pili ya mazungumzo ya kurudisha amani katika Somalia yaliyoandaliwa kufanyika Khartoum, Sudan kati yao na viongozi wa Serekali ya Mpito ya Usomali.

Hali ya mgogoro katika Mashariki ya Kati.

Alkhamisi KM Kofi Annan aliwakilisha mbele ya Baraza la Usalama, katika kikao cha hadhara, ripoti maalumu kuhusu hali katika Mashariki ya Kati, taarifa ambayo inaelezea matokeo ya juhudi za ujumbe wa maofisa watatu wa vyeo vya juu wa UM, waliozuru Mashariki ya Kati karibuni, kwa madhumuni ya kutafuta taratibu za kuridhisha kusitisha mapigano haraka na kuwasilisha suluhu inayokubalika na wote wahusika na mgogoro huo.~