Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Wakuu wa UM wanataka Wa-Kongo wasubiri matokeo rasmi

Likiwapongeza wananchi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa kushiriki katika uchaguzi wa kihistoria wa nchi yao, kwa sehemu kubwa kabisa kwa amani, siku ya Jumapili, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilitoa mwito wiki hii kuwataka wawe watulivu na kusubiri matokeo ya mwisho ya uchaguzi.

Jaribio la Mapinduzi lagunduliwa Burundi

Afisi ya kulinda amani ya UM huko Burundi ONUB imeeleza kushangazwa na ripoti kua kulikuwepo na jaribio la kuipindua serekali ya Bujumbura, siku chache zilizopita na kwamba kuna wanasiasa mashuhuri walotiwa vizuizini.

UNICEF kulaani vitendo vya ubakaji wa watoto Zimbabwe

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia watoto UNICEF limelaani vikali sana habari za kutokea vitendo zaidi vya ubakaji huko Zimbabwe na likihimiza sheria mpya kupitishwa kuwalinda watoto wa nchi hiyo na kutoa masomo zaidi juu ya virusi vua HIV na Ukimwi.

Wafanyakazi wa kimataifa washindwa kuhudumia raia muhitaji katika jimbo la Sudan la Darfur

Shirika la UM juu ya Operesheni za Amani katika Sudan, UNMIS, limeripoti karibuni ya kuwa wafanyakazi wa kimataifa wanaosimamia huduma za kiutu katika Darfur wanakabiliwa na vizingiti vinavyokwamisha huduma za kuwasaidia raia kupata mahitaji ya kunusuru maisha kwa sababu ya kuendelea kwa mashambulio na hali ya utumiaji nguvu dhidi yao, pamoja na vitendo vya uharamia na mapigano yalioshtadi kati ya makundi ya waasi.~~

Wanajeshi waangalizi wanne wa UM Kuuwawa Lebanon

Naibu KM wa Idara ya UM juu ya Operesheni za Amani Duniani, Jane Holl Lute aliripoti mbele ya Baraza la Usalama wiki hii kwamba wanajeshi waangalizi wanne wa ulinzi wa amani wasiochukua silaha kutoka Austria, Kanada, Finland ~na Uchina, waliuawa Ijumanne kwa mizinga ya majeshi ya Israel ambayo tuliarifiwa ililengwa moja kwa moja, sawia, kwenye kituo cha uangalizi cha UM karibu na mji wa Khiam, Lebanon ya kusini.

UM yaahidi kuongeza misaada ya kiutu Lebanon

Ilivyokuwa matatizo ya kiutu bado yanaendelea kukithiri katika mazingira ya vita katika Lebanon ya kusini UM umeripoti ya kuwa utalazimika kupeleka misafara ziada ya misaada ya kihali katika miji ya Jezzine na Sidon ili kukidhia mahitaji ya kunusuru maisha kwa umma waathiriwa wa maeneo haya. Hatua hii imechukuliwa baada ya msafara wa UM kufanikiwa Ijumanne kupeleka katika mji wa bandari wa Tyre shehena za chakula na mahitaji mengineyo ya kiutu.