Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Burundi itahitajia msaada wa kimataifa kujenga amani, yasema UM

Mjumbe Maalumu wa KM kwa Burundi, Nureldin Satti aliwaambia waandishi habari wa kimataifa katika Makao Makuu ya kwamba licha ya kuwa Shirika la Ulinzi wa Amani la UM katika Burundi (ONUB) litamaliza operesheni zake mwisho wa mwezi Disemba hatua hiyo haimaanishi mchango wa kimataifa hauhitajiki tena.

Mahakama ya ICTR yataka hukumu ya Seromba irekibishwe

Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya UM juu ya Rwanda (ICTR) amependekeza hukumu ya kifungo cha miaka 15 aliopewa Athanase Seromba karibuni ibadilishwe kwa sababu anaamini mtuhumiwa huyo aliyekuwa padri wa Parokia ya Nyange, katika kijiji cha Kivumu alishiriki kwenye makosa ya jinai ya hali ya juu iliyohusika na mauaji ya halaiki. Kwa hivyo, Mwendesha Mashitaka angelipendelea Seromba anapewa adhabu kali zaidi.

Mukhtasari juu ya Mkutano Mkuu wa Pili kuhusu Maziwa Makuu

Mkutano Mkuu wa Pili juu ya Maziwa Makuu ulioandaliwa shirika na UM pamoja Umoja wa Afrika (AU), na kuhudhuriwa na Viongozi sita wa Taifa na Mkuu mmoja wa Serekali, wakiwakilisha mataifa ya Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC), Uganda, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rwanda na Kenya ulifanyika wiki hii mjini Nairobi.

Baraza la Haki za Kiutu kutuma ujumbe wa uchunguzi Darfur

Baraza la UM juu ya Haki za Kiutu wiki hii mjini Geneva limepitisha, kwa kauli moja, azimio la kupeleka ujumbe maalumu wa watu watano wa hadhi ya juu, katika jimbo la Darfur, Sudan ili kutathminia na kusailia hali ambayo imeripotiwa kufurutu ada katika utekelezaji wa haki za kimsingi kwa raia.

Chuo Kikuu cha Pretoria kutunukiwa zawadi ya UNESCO

Kitivo cha Haki za Kiutu cha Chuo Kikuu cha Pretoria, Afrika Kusini kinachosimamia mafunzo yanayohusu taratibu za kuimarisha haki za kimsingi kimetunukiwa zawadi ya dola 10,000 na Shirika la Umoja wa Mataifa juu ya Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO).