Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mukhtasari juu ya Mkutano Mkuu wa Pili kuhusu Maziwa Makuu

Mukhtasari juu ya Mkutano Mkuu wa Pili kuhusu Maziwa Makuu

Mkutano Mkuu wa Pili juu ya Maziwa Makuu ulioandaliwa shirika na UM pamoja Umoja wa Afrika (AU), na kuhudhuriwa na Viongozi sita wa Taifa na Mkuu mmoja wa Serekali, wakiwakilisha mataifa ya Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC), Uganda, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rwanda na Kenya ulifanyika wiki hii mjini Nairobi.

Sikiliza taarifa kamili pamoja na mahojiano na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania, Dktr Asha-Rose Migiro kwenye redio ya mtandao.