Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Njia za kudumisha amani na maendeleo nchini Somalia

Mjumbe maalum wa Katibu mkuu huko Somalia Bw Francois Fall alikutana na kundi la wajumbe wa kimataifa linalo jaribu kutafuta njia za kudumisha amani na maendeleo katika taifa hilo la pembe mwa afrika na kujadili njia za kuimarisha msaada wa kimataifa katika juhudi zao

Wagombea urais nchini DRC wakubali kuunda tume

Afisi ya Umoja wa mataifa huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, MONUC ilitangaza wiki hii kuwa wagombea wawili walobaki wa kiti cha rais huko kutokana na uchaguzi wa mwezi uliyopita, wamekubaliana kuunda tume ya pamoja kuchunguza ghasia zilizotokea baada ya kutolewa matokeo ya awali,

Sudan kupata huduma za afya kutoka serikali ya Japan

Akina mama na watoto wa kaskazini mwa Sudan watafarijika hivi sasa kwa kuweza kupata machanjo muhimu ya kuokoa maisha na madawa ya malaria pamoja na huduma za afya kutokana na msaada kutoka serekali ya Japan wa dola milioni 4.5 ulokabidhiwa UNICEF. Shirika la watoto linaeleza kua msaada huo utasaidia kuimarisha afya ya kiasi ya watu milioni 3 na nusu.

Haki za walemavu

Wiki hii kwenye Umoja wa Mataifa wajumbe kutoka pembe zote za dunia wanakutana hapa New York katika juhudi za kukamilisha mkataba wa kimataifa juu ya haki za walemavu.

UKIMWI - Mkutano wa Toronto

Suala la wanawake na watoto ilipewa kipaumbele kwenye mazungumzo ya Toronto, hasa kulitolewa mwito kuwapatia wanawake mamlaka zaidi ili waweze kujikinga kutokana na ghasia na tumiaji nguvu dhidi yao.