Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Haki za walemavu

Haki za walemavu

Wiki hii kwenye Umoja wa Mataifa wajumbe kutoka pembe zote za dunia wanakutana hapa New York katika juhudi za kukamilisha mkataba wa kimataifa juu ya haki za walemavu.

TYMnaendelea kusikiliza makala ya Jarida kutoka redio ya Umoja wa Mataifa. Abdushakur Aboud anaripoti juu ya mkutano huo.

AA.kamishna mkuu wa haki za binada wa umoja wa mataifa Bi Louise Arbour amesema ataunga mkono mkataba wa kimataifa utakao Linda haki za walemavu. Akizungumza jana kwenye mkutano huo alisema viwango vya haki za binadam vilivyoko hivi sasa pamoja na taratibu hazitoshi na hazikidhi mahitaji ya walemavu matokeo yake anasema bi Arbour anasema kiasi ya asili mia 10 ya wakazi wa dunia wanakabiliwa na hali mbaya kabisa ya ukiukaji na kunyimwa haki msingi za binadam. Mjumbe kutoka Zanzibar, Bi Zulegha Yunus Haji anasema mkutano una faida kwani unawapatia nafasi ya kujadili masuala mbele ya bunge za nchi zao.

Bi Zulegha Haji:

Suala la haki za wanawake kwa kawaida hupatiwa umuhimu mkubwa katika majadiliano kama haya na Bi Zulegha Haji anasema anahisi elimu ni jambo muhimu kabisa kuweza kutetea haki zao.

Bi Zulegha Haji:

AA: Mkataba huo ukidihinishwa utakua wa kwanza kabisa juu ya haki mpya za binadam katika karne hii ya 21 na hivyo kubadili kabisa jinsi karibu watu milioni 650 duniani wanavyo tendewa. Mkataba huo unatazamiwa kukamilishwa hii leo na utazilazimisha mataifa miongoni mwa mambo mengi kufanya mabadiliko ya kuwawezesha walemavu kuingia na kutoka katika majengo mepya na kuimarisha elimu na habri juu ya haki zao na kuondowa kabisa hali ya unyanyasaji dhidi ya walemavu.