Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Hapa na Pale

Mwigizaji maarufu wa michezo ya sinema Marekani, Ben Affleck ambaye pia ni mwongozaji filamu, akijumuika na mwimbaji wa kundi la Rolling Stone, Mick Jagger, leo wamewasilisha rasmi filamu fupi ilionyeshwa Makao Makuu ya UM mjini New York, inayoitwa “Nipe Hifadhi ya Makazi/Gimme Shelter”, kwa lengo la kuchangisha fedha za kuwasaidia kihali wahamiaji 250,000 katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (JKK), waliong’olewa makwao baada ya kufumka mapigano katika eneo la mashariki. UM unahitajia kufadhiliwa msaada wa dola

Mastakimu ya muda yanaandaliwa Sudan Kusini na UNHCR kwa wahamiaji wa JKK

Katika taarifa nyengine, UNHCR inajiandaa kupokea wahamiaji wanaolekea Sudan Kusini hivi sasa, kufuatia ripoti za kuanzishwa operesheni za pamoja za kijeshi zilizojumuisha vikosi vya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Uganda na kutoka Sudan Kusini, askari ambao wana lengo la kuwafyeka kutoka mafichoni waasi wa Uganda wa kundi la LRA, waliojizatiti kwenye maeneo yaliopo kaskazini-mashariki ndani ya JKK, kwenye Mbuga ya Taifa ya Garamba.

Hapa na Pale

Ijumanne alasiri Baraza la Usalama limepitisha azimio, liliothibitisha wazi kuunga mkono majadiliano yalioanzishwa mwaka jana kwenye mji wa Annapolis, Maryland, Marekani kuhusu suala la amani baina ya Waisraili na WaFalastina. Vile vile azimio limeahidi kuhakikisha mazungumzo ya pande mbili, baina ya Waisraili na WaFalastina, hayatotenguliwa wala kubadilishwa. Azimio liliodhaminiwa bia na Marekani na Urusi lilipitishwa na mataifa 14 kati ya wajumbe 15 wa Baraza. Libya iliamua kutopiga kura.