Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa Maji kwa Kilimo na Nishati kwa Afrika wakamilisha majadiliano Sirte

Mkutano wa Maji kwa Kilimo na Nishati kwa Afrika wakamilisha majadiliano Sirte

Mkutano wa siku tatu kuzingatia ‘Utunzaji wa Maji kwa Kilimo na Nishati katika Afrika’, uliofanyika kwenye mji wa Sirte, Libya, kuanzia Ijumatatu tarehe 15 Disemba na kuongozwa na Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO), umehitimishwa leo Ijumatano, Disemba 17, 2008.

“Kwanza naona huu mkutano, kongomano hii inaendelea hapa mjini wa Sirte, hapa Libya, inakua ya maana sana kwa sababu tunaongea juu ya vile tunaweza kusaidia wananchi kutoka kwa taifa zetu, tunaongea sana juu ya vile wanaweza

kusaidiwa kwa mambo ya chakula. Kwanza, tuone vile tunaweza kusaidia wananchi wapate chakula saa hii, kwa sababu kuko na ukosefu wa chakula kila pahali nchini zetu. Hii inaitwa food crisis ambao tunaiona ya kwamba wananchi hawawezi wakapata chakula ya kutosha, na hiyo ndio FAO wametuleta pamoja ili tuone vile tunaweza kufikiria, tutafute namna, tutafute mbinu ya kuwapatia wananchi wetu au watu kutoka kwa kila nchi chakula.”

Taarifa rasmi ya Mkutano wa Sirte, iliotolewa baada ya majadiliano kumalizika, imewakilisha Azimio la Mwito ulioahidi kwamba mataifa ya Afrika yatafanya kila yawezalo, kwa kulingana na uwezo wao, kuitekeleza miradi ya kukuza huduma za maji, kikamilifu, ili kuimarisha kilimo na kuzalisha nishati maridhawa inayotumia nguvu ya maji katika bara la Afrika.