Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Mradi wa Mbola kupiga vita umasikini kwa kuwaridhisha madaraka wanakijiji

Mradi wa Umoja wa Mataifa wa Vijiji vya Milenia (MVP) unaotekelezwa kwenye Kijiji cha Mbola, Tanzania unajitahidi kuwasaidia wanakijiji kupatiwa madaraka na uwezo wa kujiamulia taratibu zinazofaa kuhudumiwa kupunguza umasikini na hali duni kwenye eneo lao. Huduma hizi huongozwa na wataalamu wa fani mbalimbali ambao huwasaidia wanakijiji kupata ujuzi unaowaletea natija za kiuchumi na, hatimaye, kuwavua na janga la umasikini na ufukara. Katika kipindi tumebahatika kujumuisha maoni ya mwanakijiji Christina Mabula pamoja na Anna Linje, mwanafunzi mtafiti wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine, kiliopo Morogoro, Tanzania ambayo yanazingatia juhudi zinazotakikana kuimarisha kipamoja maendeleo ya kijijini katika Mbola.

Mradi wa Mbola kupiga vita umasikini kwa kuwaridhisha madaraka wanakijiji

Mradi wa Umoja wa Mataifa wa Vijiji vya Milenia (MVP) unaotekelezwa kwenye Kijiji cha Mbola, Tanzania unajitahidi kuwasaidia wanakijiji kupatiwa madaraka na uwezo wa kujiamulia taratibu zinazofaa kuhudumiwa kupunguza umasikini na hali duni kwenye eneo lao. Huduma hizi huongozwa na wataalamu wa fani mbalimbali ambao huwasaidia wanakijiji kupata ujuzi unaowaletea natija za kiuchumi na, hatimaye, kuwavua na janga la umasikini na ufukara. Katika kipindi tumebahatika kujumuisha maoni ya mwanakijiji Christina Mabula pamoja na Anna Linje, mwanafunzi mtafiti wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine, kiliopo Morogoro, Tanzania ambayo yanazingatia juhudi zinazotakikana kuimarisha kipamoja maendeleo ya kijijini katika Mbola.

KM atathminia shughuli za UM kwa 2008

KM Ban Ki-moon alikutana na waandishi habari mwanzo wa wiki na aliwasilisha ajenda aliyopendekeza ijumuishwe katika kazi za UM katika mwaka 2008. KM Ban alisema kwenye risala yake ya ufunguzi kwamba atatumia wadhifa wake kuhakikisha 2008 utakaobarikiwa mchango ziada kutokana na bidii ya kimataifa katika kukabiliana na masuala yanayohusu mabadiliko ya hali ya hewa duniani na pia ulinzi wa amani ya kimataifa.~~

Mashirika ya UM yaendelea kuhudumia misaada ya kiutu Kenya

UM na mashirika yake mbalimbali yaliopo Kenya yanashiriki kwenye huduma kadha wa kadha za kukidhi mahitaji ya umma ulioathiriwa na machafuko yaliyofumka karibuni nchini Kenya baada ya uchaguzi kumalizika. Kwa mujibu wa taarifa ya Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) misaada hii hugaiwa na kuenezwa kwenye maeneo muhitaji na mashirika ya UM, mathalan UNHCR, WFP na UNICEF, hususan katika lile eneo la Kaskazini la Mkoa wa Bonde la Ufa/Northern Rift Valley.

Uchumi wa dunia kwa 2008 unakabiliwa na hatari ya mzoroto, kuonya UM

Wiki hii UM uliwasilisha ripoti maalumu katika Makao Makuu New York na vile vile kwenye ofisi zake ziliopo mjini Geneva, ambayo ilizingatia na kutabiri hali ya uchumi duniani katika 2008. Ripoti ilitayarishwa shirika na Idara ya UM juu ya Masuala ya Uchumi na Jamii (DESA) pamoja na Shirika la Maendeleo na Biashara (UNCTAD).

DPKO inakhofia wanajeshi wa UNAMID hawatoenezwa Darfur kwa wakati

Jean-Marie Guehenno, Mkuu wa Idara ya UM juu ya Operesheni za Ulinzi wa Amani Duniani (DPKO), alikuwa na mashauriano maalumu na wajumbe wa Baraza la Usalama kuhusu vizingiti vilivyoibuka kwenye juhudi za kukamilisha upelekaji wa vikosi mseto vya UNAMID katika jimbo la Darfur, Sudan magharibi. Vikosi vya UNAMID vinategemea mchango wa wanajeshi wa Umoja wa Mataifa (UM) na Umoja wa Afrika (UA).

Kesi ya aliyekuwa raisi wa Liberia imeanza kusikilizwa tena mjini Hague

Kesi ya raisi wa zamani wa Liberia Charles Taylor imeanza kusikilizwa tena mapema wiki hii kwenye mji wa Hague, Uholanzi baada ya kuakhirishwa kwa muda wa miezi minne ili kuwasaidia mawakili wa mshitakiwa muda zaidi wa kutathminia kurasa 40,000 za ushahidi zilizoandaliwa na wanaoendesha mashtaka. Kesi inasimamiwa na Mahakama Maalumu juu ya Makosa ya Vita katika Sierra Leona (SCSL) ambayo husaidiwa na inaungwa mkono na UM. Taylor ametuhumiwa makosa 11 yanayoambatana na jinai ya vita - ikijumuisha mchango wake katika mauaji ya halaiki, ukataji wa viungo unaolemaza kwa wapiganaji, utumwa wa kiasherati na kijinsia, na pia ushirikishaji wa nguvu wa watoto wadogo kwenye mapigano. Tuhumza hizi zinahusikana na vurugu liliozuka katika Sierra Leone kwa muda wa miaka kumi, taifa ambalo ni jirani na Liberia. Taylor amekana makosa yote dhidi yake.

Mazungumzo ya upatanishi juu ya Sahara ya Magharibi yamemalizika, yatarudiwa tena Machi

Duru ya tatu ya mazungumzo ya siku mbili yalioandaliwa na UM kutafuta suluhu ya kuridhisha juu ya tatizo la Sahara ya Magharibi, yaliofanyika kwenye mji wa Manhasset, katika Jimbo la New York yamemalizika kati ya wiki. Makundi yote husika na mzozo huu yalitoa taarifa ya pamoja baada ya mkutano kukamilishwa iliosema makundi husika yamekubaliana kukusanyika tena mwezi Machi mahali hapo hapo pa Manhasset na yameahidi kuwa yazingatia kwa hamasa zaidi na kiwango kikubwa yale masuala yaliotatanisha upatanishi wao.

UM yahudumia misaada ya kiutu kwa waathiriwa wa mafuriko kusini ya Afrika

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) ikishirikiana na jumuiya zisio za kiserekali imo mbioni kuhudumia mataifa ya kusini ya Afrika kupata misaada ya kihali kuwavua makumi elfu ya raia katika Msumbiji, Zambia na Zimbabwe na hatari iliozuka karibuni katika eneo lao, baada ya mvua kali kunyesha nje ya majira ya kawaida na kusababisha Mto Zambezi kufura kwa kasi na kueneza mafuriko.