Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kesi ya aliyekuwa raisi wa Liberia imeanza kusikilizwa tena mjini Hague

Kesi ya aliyekuwa raisi wa Liberia imeanza kusikilizwa tena mjini Hague

Kesi ya raisi wa zamani wa Liberia Charles Taylor imeanza kusikilizwa tena mapema wiki hii kwenye mji wa Hague, Uholanzi baada ya kuakhirishwa kwa muda wa miezi minne ili kuwasaidia mawakili wa mshitakiwa muda zaidi wa kutathminia kurasa 40,000 za ushahidi zilizoandaliwa na wanaoendesha mashtaka. Kesi inasimamiwa na Mahakama Maalumu juu ya Makosa ya Vita katika Sierra Leona (SCSL) ambayo husaidiwa na inaungwa mkono na UM. Taylor ametuhumiwa makosa 11 yanayoambatana na jinai ya vita - ikijumuisha mchango wake katika mauaji ya halaiki, ukataji wa viungo unaolemaza kwa wapiganaji, utumwa wa kiasherati na kijinsia, na pia ushirikishaji wa nguvu wa watoto wadogo kwenye mapigano. Tuhumza hizi zinahusikana na vurugu liliozuka katika Sierra Leone kwa muda wa miaka kumi, taifa ambalo ni jirani na Liberia. Taylor amekana makosa yote dhidi yake.