Wakazi wa Nzara Sudan Kusini waathiriwa na moto wa nyika-UNMISS
Wakati Sudan kusini ikiendelea kupambana kuimarisha amani, wakazi wa eneo la Nzara wamekumbwa na janga la moto wa nyika ambao umeteketeza takribani maili tano za mraba katika jimbo la Equatoria Magharibi na kuwaacha mamia ya watu bila makazi umesema mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNMISS.