Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Sudan Kusini

Mwanamke mmoja katika kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa akiwa amevaa yunifomu ya kujificha na kofia ya chuma ya bluu akichukua mtoto mwenye tabasamu huku amesimama mbele ya makao ya muda pamoja na wanawake wawili wa eneo hilo huko Bentiu, Sudan Kusini.
UNMISS

Siku katika maisha ya kazi ya Wafaa, Afisa Polisi wa UNMISS

Mji wa Bentiu ulioko Kaskazini mwa Sudan Kusini ni eneo linalokumbwa na mafuriko yanayoharibu makazi na migogoro inayowafanya maelfu ya watu kuishi kwenye kambi za wakimbizi. Katika mazingira haya magumu, Afisa wa Polisi wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, UNMISS, Wafaa Assri Sameeh Al-Goussous kutoka nchini Jordan, anafanya kazi ya kujenga uaminifu na uhusiano madhubuti kati ya jamii na vyombo vya dola kupitia doria na mafunzo. Rashid Malekela anatupeleka huko kufahamu maisha ya kila siku ya Afisa Wafaa yakoje.

Sauti
3'12"
Mwanamke wa Sudan Kusini akipika chakula shuleni kwenye sufuria kubwa juu ya moto ulio wazi huko Akobo Magharibi, Jimbo la Jonglei, Sudan Kusini.
WFP

UN yatoa tamko kufuatia amri ya jeshi la Sudan Kusini kuyataka mashirika ya kutoa misaada kuondoka Akobo

Timu ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia Masuala ya Kibinadamu nchini Sudan Kusini imeeleza wasiwasi wake mkubwa kufuatia amri iliyotolewa na Jeshi la ulinzi la wananchi wa Sudan Kusini (SSPDF) tarehe Machi 6, 2026, inayoyataka Mashirika ya Misaada ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa na yale ya kiraia kuondoka katika eneo la Akobo, kusini mwa jimbo la Jonglei kupisha operesheni za kijeshi.