COVID-19 isiwe chanzo cha kusahau huduma muhimu za chanjo kwa watoto- UNICEF
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limesihi serikali duniani kote kuanza mipango thabiti ya utoaji chanjo kwa watoto pindi janga la ugonjwa wa virusi vya Corona, au COVID-19 litakapodhibitiwa.