Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Njaa inatumiwa kama mbinu ya vita huko Sudan Kusini - Jopo la UN 

Familia iliyotawanywa ikiondoka katika kambi ya ulinzi wa raia ya Umoja wa Mataifa mjini Juba kurejea nyumbani kwao Jonglei Sudan Kusini
UN Photo/Isaac Billy
Familia iliyotawanywa ikiondoka katika kambi ya ulinzi wa raia ya Umoja wa Mataifa mjini Juba kurejea nyumbani kwao Jonglei Sudan Kusini

Njaa inatumiwa kama mbinu ya vita huko Sudan Kusini - Jopo la UN 

Haki za binadamu

Ripoti yenye kurasa 46 iliyotolewa leo mjini Geneva Uswisi na tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNCHRSS, imeeleza kuwa Sudan Kusini tangu ilipopata uhuru wake mwaka 2013, mzozo wa kikatili nchini humo umesababisha mateso yasiyoweza yasiyopimika kwa raia na kusababisha kiwango viwango vya kutisha vya ukosefu wa chakula na utapiamlo hali ambayo inatumiwa kama mbinu ya vita. 

"Pamoja na watu milioni 7.5 wa Sudan Kusini wanaohitaji msaada wa kibinadamu kwa sasa, tumegundua kwamba uhaba wa chakula katika Bahr el Ghazal Magharibi, Jonglei, na Jimbo la Ikweta ya Kati umeunganishwa moja kwa moja na mzozo huo na kwa hivyo karibia umesababishwa kabisa na wanadamu," amesema Mwenyekiti wa Tume, Yasmin Sooka. 

Yasmin ameongeza akisema, “ni wazi pande zote mbili yaani serikali na vikundi vya upinzani vimetumia kwa makusudi njaa ya raia kama mbinu ya kivita katika majimbo haya, wakati mwingine kama  zana ya kuadhibu jamii ambazo haziwauni mkono kama vile Jonglei.”  

Ripoti hiyo ya aina yake inaeleza namna ambavyo kati ya mwezi Januari 2017 na Novemba 2018, vikosi vya Serikali kwa makusudi ilinyima jamii ya Fertit na Luo wanaoishi chini ya udhibiti wa upinzani katika Jimbo la Bahr el Ghazal Magharibi la rasilimali muhimu, kwa vitendo vinavyojumuisha adhabu ya pamoja na njaa kama njia ya vita, ripoti imegundua. Makamanda wa serikali pia waliidhinisha wanajeshi wao kujipatia kujizawadia wenyewe kwa kupora vitu muhimu  kwa uhai wa watu hawa wa vijijini. 

Kamishina Andrew Clapham amesema, “mashambulio endelevu yalitekelezwa dhidi ya miji na vijiji vingi kote Jimbo la Bahr el Ghazal Magharibi kwa miaka kadhaa, ambayo yalisababisha idadi kubwa ya vifo, ubakaji, na uharibifu, uchomaji moto, na uporaji wa mali, ukosefu wa chakula uliosababishwa ulizidisha ukosefu wa usalama wa mwili, na kuwaacha raia hawana njia nyingine ila kukimbia.” 

Kwa upande wake Kamishina Barney Afako amesisitiza kuwa, “Bila utekelezaji wa wakati unaofaa wa mchakato wa haki ya mpito jumishi, kama inavyoelezwa katika mkataba wa amani, amani endelevu kwa Sudan Kusini itaendelea kutoweka.”